Na:
Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Serikali
imeamuru kurudishwa kazini kwa Watumishi wote ambao walikuwa na ajira za kudumu
au ajira za mikataba (kwa watendaji wa Vijiji na Mitaa) au ajira za muda ambao
walikuwa kazini kabla ya Mei 20, 2004 ulipoanza kutumika waraka wa Utumishi Na.
1 wa mwaka 2004 ambao umetaja kuwa cheti cha ufaulu wa mtihanai wa kidato cha
nne kama sifa ya msingi kwa mtumishi wa Umma.
Kauli
hiyo imetolewa leo bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika
alipokuwa akitoa Kauli ya serikali kuhusu watumishi waliondolewa kwenye mfumo
wa malipo ya mshahara kwa kukosa sifa ya cheti cha kufaulu mtihani wa elimu ya
kidato cha nne.
"Watumishi
wa Umma Elfu Moja Mia Tatu Sabini (1,370) waliolegezewa masharti ya sifa za
muundo kupitia barua ya Katibu Mkuu Utumishi yenye Kumb. Na.
CCB.271/431/01/p/13 ya tarehe 30 Juni, 2011 warejeshwe kazini mara moja,
walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na
waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa mujibu wa Sheria," alisema
Mhe. Mkuchika.
Hata
hivyo amesema kuwa uamuzi huu uliotajwa hautawahusu watumishi wawasilisha vyeti
vya kughushi katika kumbukumbu za ajira zao, watumishi waliokuwepo katika ajira
kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 pamoja na warumishi wote walioajiriwa baada ya
tarehe 20 Mei 2004 wakiwa hawana sifa za kufaulu mtihani wa kidato cha nne kwa
kuwa walijipatia ajira kinyume cha maelekezo ya Serikali.
Aidha,
watendaji wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi wote walioshiriki kuwaajiri
Watumishi wasiokuwa na sifa ya kufaulu mtihani wa kidato cha nne katika
Utumishi wa Umma baada ya tarehe 20 Mei, 2004 watachukuliwa hatua za kinidhamu
kwa mujibu wa sheria, kanuni za taratibu.
Vilevile
watendaji wakuu na maafisa wote wanaosimamia zoezi hili ambao kwa namna yoyote
ile watashiriki kuhujumu zoezi hili kwa kuondoa au kuharibu kumbukumbu za
Watumishi ili haki isitendeke, watachukuliwa hatua za kinidhamu na za kijinai
ikibidi.
0 comments:
Post a Comment