Home » » 'HATI IWEHALISI AU SIYO,MJADALA UFUNGWE'

'HATI IWEHALISI AU SIYO,MJADALA UFUNGWE'

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Maria Sarungi ameomba mjadala kuhusu Hati ya Muungano ufungwe hata kama itakayowasilishwa bungeni haitakuwa halisi.
Mjadala huo uliubuka bungeni kuanzia kwenye kamati, baadhi ya wajumbe wakidai sahihi za hayati Mwalimu Nyerere na aliyekuwa Katibu wa Bunge, Pius Msekwa zimegushiwa.
Alisema hayo bungeni, akichangia mjadala wa sura ya kwanza na ya sita zinazohusu Muungano.
Alisema ni muumini wa Muungano imara unaozingatia historia.
“Badala ya kurushiana maneno, tuamue jinsi ya kuboresha Rasimu kwani inachohitaji ni kuboreshwa,” alisema Maria.
Alishauri upatikane wakati mwafaka wa kujadili Muungano wa sasa na kwamba suala la hati lifungwe bila kujali kuwa itakayopelekwa itakuwa halisi au siyo.
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa