Home » » WAMACHINGA WANAOFANYA KAZI ZAO KWENYE VITUO VYA DALADALA NA MABASI SASA KUONDOLEWA‏

WAMACHINGA WANAOFANYA KAZI ZAO KWENYE VITUO VYA DALADALA NA MABASI SASA KUONDOLEWA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma SSP Peter Simaakifafanua jambo  alipokuwa akizungumza na madiwani wa manipaa ya Dodoma lililofanya mwishoni mwa wiki hii.
 Meya wa Manispaa ya Dodoma Emanuel Mwiliko akifafanua jambo kwenye baraza la madiwani lililokutana mwisho wa wiki kujadili juu ya makusanyo mbalimbali ili kukamili makadilio ya mwaka huu wa fedha, kushoto ni Naibu Meya Jumanne Ngede.

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Robert Kitimbo akielezea jambo katikakikao cha baraza la madiwani  alipokuwa akiwataarifu kukabidhi ofisi ambako atakufanya julai 7 mwaka huu baada ya kustaafu, waliokaa ni Meya wa manispaa hiyo Emanuel Mwiliko, Naibu Meya Jumanne Ngede na
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Dkt David Malole.
Madiwani wa Manispaa wa Dodoma wakiwa katika ukumbi wa manispaa wakifuatilia jambo wakatiwalipokuwa kwenye baraza la kawaida la kujadili makusanyo ya mwaka wa fedha kwa kiasi walichofikisha mpaka hivi sasa ambapo zimebaki siku chache ili kuyawakilisha serekali kuu.

Na John Banda, Dodoma
IMEELEZWA kuwa kitendo cha wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) kuzagaa sehemu za watembea kwa miguu katika maeneo ya stendi ni hatari inayoweza kuwasababishia ajali wakati wowote.
Kauri hiyo ilitolewa na Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Dodoma SSP Peter Sima kwenye baraza la madiwani lilifanyika jana.
Sima alisema machinga hao ambao huuza bidhaa mbalimbali zikiwemo za masokoni katika sehemu hizo za watembea kwa miguu wakati wowote wanaweza kusababisha ajali kutokana na watembea kwa miguu kushindwa kupita na badala yake huwalazimu kupita kwenye barabara.
Alivitaja vituo hivyo kuwa ni kile cha Daladala jamatini, stendi ya mkoa (oil com) naya magali ya vijijini ya Mshikamano ambako wamachinga hao huzagaa bila hata kujali usalama wao.
Aidha aliwataka manispaa kuhakikisha wanawaelekeza machinga hao pakufanyia biashara zao lakini badala ya kuwaacha katika maeneo hayo ambayo ni hatari kwa maisha yao.
‘’Mhe. Meya hakikisheni wamachinga hao wanaondoka katika maeneo hayo kwa ajili ya usalama wao na kuuwema mji safi wenye muonekano wa kuwa jiji la sivyo tutawaondoa kwa nguvu kutokana na sheria
zinavyotuelekeza’’, alisema Sima
Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu kati ya machinga hao ambao wengi wao hukimbia masokoni wakijazana kwenye vituo hivyo bila utaratibu na watendaji wa manispaa ambao wanaonekana kuwashindwa maana wamekuwa wakiachwa kuzagaa hovyo huko wakichafua madhingira katika maeneo hayo
bila kuchukuliwa hatua yoyote.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa