Home » » ASKOFU AKEMEA WABUNGE KUZOMEANA

ASKOFU AKEMEA WABUNGE KUZOMEANA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

ASKOFU wa Kanisa la The Gospel Ministry, Kanda ya Kati, Christopher Madole, amekemea wabunge kutumia muda wao kuzomeana na kutukanana badala ya kujadili hoja.
Akizungumza na Tanzania Daima jana juu ya mwenendo wa Bunge, alisema inasikitisha kuona wabunge badala ya kujadili hoja wanajikita katika malumbano ambayo hayawasaidii Watanzania.
Alisema kwa sasa umeanzishwa mtindo wa baadhi ya wanasiasa au jamii kutumia mitandao ya kijamii kuchafuana, jambo ambalo linatia aibu katika jamii.
“Sawa kwa sasa ni kipindi cha utandawazi, lakini inasikitisha kuona mitandao ya kijamii ikitumiwa vibaya kwa kuweka picha za viongozi wakiwa watupu, jambo ambalo ni aibu kwa taifa,” alisema.
Akizungumzia maadili ya Kitanzania, Askofu Madole alisema serikali inatakiwa kuwa macho katika kudhibiti mambo ambayo hayapendezi katika jamii, ikiwa ni pamoja na kuwapa onyo kali wale wote ambao wanatumia vibaya mitandao ya kijamii
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa