Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Alhaj Adam Kimbisa wa kwanza kulia na Mwenyekiti wa ccm wilaya ya kondoa
anaefuatia kutoka kulia wakisikiliza burudani za vikundi mbambali
wakati wa ziara yake wilayani Kondoa
Kushoto ni Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Dodoma Alhaj Adam Kimbisa,
akifuatiwa na Mbunge wa Kondoa kaskazini wakicheza ngoma ya asili ya
warangi wilayani Kondoa wakati wa ziara ya siku mbili ya mwenyekiti huyo
wa CCM mkoa wa Dodoma.
Jembe la sera CCM, Haji Manara akiwaweka sawa wananchi wa kijiji cha
Kinyasi wilayani Kondoa kabla ya mwenyekiti CCM mkoa kuwahutubia
wananchi hao wakati wa ziara yake ya siku mbili wilayani humo,iliyoanza
juzi na kumalizika jana.
Mkuu wa wilaya ya Kondoa Omary Kwaang' akisikiliza kwa makini moja kati
ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wananchi wa kijiji cha Kinyasi
kuhusiana na mgogoro wa Ardhi na mipaka kati ya wananchi na serikali.
Na. Bilson Vedastus - Dodoma
Hatimaye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Dodoma Alhaji
Adam Kimbisa amehitimisha ziara yake ya zaidi ya siku 28 kutembelea
wilaya saba za mkoa wa Dodoma kwa lengo la kukagua na kuimarisha uhai wa
chama kwa kipindi cha miaka minne kabla ya kuelekea uchaguzi mkuu huku
akiahidi kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo mgogoro wa mpaka kati ya
hifadhi ya Mkungunero na Ardhi inayotumiwa na wananchi wa vijiji kumi
vinavyozunguka hifadhi hiyo iliyopo kata ya Kinyasi wilayani Kondoa
mkoani Dodoma
Akiwa wilayani Kondoa Alhaji Kimbisa amesema atazungumza na viongozi wa
idara husika pamoja na kumuona waziri mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda ili
hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya mgogoro huo
Aidha Alhaji Kimbisa aliwaomba wananchi kuwa watulivu wakati ccm
wakifanyia kazi mgogoro huo wakishirikiana na mkuu wa wilaya hiyo ili
kupata haki ya pande zote mbili.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kondoa Omary Kwaang amekiri kuwepo kwa
mgogoro huo ambao umedumu tangu mwaka 2006 baada ya wataalamu kuanza
kupima hali ambayo mwaka 2007 ilisababisha askari kuuwawa ambapo amesema
zaidi ya mara mbili kwa barua na maongezi ya ana kwa ana viongozi wa
wilaya ya kondoa wamelifikisha swala hilo kwa vyombo husika ikiwemo
wizara ya Ardhi,Tamisemi na serikali kuu lakini hadi leo hakuna ufumbuzi
wowote juu ya tatizo hilo
Mmoja wa waathirika wa mgogoro huo kwa upande wa wananchi
aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhan Ally akizungumza na Nyemo fm
habari alisema chanzo cha mgogoro huo ni kubadilishwa kwa mipaka
iliyowekwa tangu enzi za mwalimu Nyerere ambapo sasa serikali
imebadilisha mipaka hiyo na kusababisha kuingilia haki ya wananchi hao.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma,Adam Kimbisa
kabla ya kuzungumza na hadhara ya wananchi alikaa na wazee wa kondoa
mjini ambao katika maongezi wao walilalamikia uhaba wa maji na kusema
hali hiyo inakwamisha maendeleo yao kwa ujumla.
Wazee hao pamoja na vingozi wa dini mbalimbali walifikisha malalamiko
hayo siku moja kabla ya mwenyekiti kufanya mkutano wa hadhara wilayani
Kondoa uliohusisha kata za Chemchem,Kondoa mjini na Kilimani wakati
walipokuwa wakizungumza nae ndani ya ukumbi wa CCM wilayani Kondoa.
Mbunge wa jimbo hilo la Kondoa Kaskazini Zabeini Mhita pia alikiri
kuwepo kwa tatizo hilo na kwamba tayari hatua za mwanzo zinaendelea
ambapo amewasilisha bungeni mahitaji ya fedha zitakazosaidia kuondoa
miundombinu mobovu na iliyochakaa sambamba na kusambaza miundombinu
mipya ili kuondoa tatizo hilo.
Hata hivyo Zabein amesema serikari inatakiwa kutambua kuwa kuna ongezeko
la watu ndani ya wilaya hiyo kwani inakuwa na watu wanazaliwa hivyo ni
vema kukapanuliwa miundombinu ya maji iatakayoendana na ongezeko la
watu.
Aidha mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma akikamilisha ziara yake ya siku
mbili kwa kila jimbo mkoani Dodoma akianzia wilaya ya
Mpwapwa,Kongwa,Chamwino,Dodoma mjini,Bahi,Chemba na kutamatisha na
Kondoa amesema atahakikisha anashugulika ili kutatua kero za wananchi
kadri ya uwezo wake kwa kushirikiana na idara husika ndani ya serikali
bila kujali itikadi za dini, vyama vya siasa na ukabila.
Alihaji Adam Kimbisa katika ziara yake ndani ya wilaya ya Chemba na
Kondoa aliambatana na Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Dodoma Donard
Simango Mejitii,aliyewahi kuwa Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es
salaam Haj Manara, Mbunge wa jimbo la Kondoa kaskazini Zabein Mhita,
Mkuu wa wilaya ya Kondoa na viongozi mbalimbali wa Chama cha mapinduzi
CCM na serikali.
Home »
» MWENYEKITI WA CCM MKOA WA DODOMA AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU 28 KWA KUTEMBELEA WILAYA ZOTE 7 MKOANI HAPO.
0 comments:
Post a Comment