Home » » UDOM YALIPA DENI LA SHS. MILIONI 63 ikiwa ni malipo ya kusimamia mitihani ya muhula uliopita ya wahadhiri wa Shule ya Sanaa na Sayansi za Jamii waliogoma na kukwamisha mitihani ya muhula huu iliyotakiwa kuanza mapema wiki hii‏

UDOM YALIPA DENI LA SHS. MILIONI 63 ikiwa ni malipo ya kusimamia mitihani ya muhula uliopita ya wahadhiri wa Shule ya Sanaa na Sayansi za Jamii waliogoma na kukwamisha mitihani ya muhula huu iliyotakiwa kuanza mapema wiki hii‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Chuo kikuu cha Dodoma


Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) umelipa madeni ya zaidi ya Sh. milioni 63 ikiwa ni malipo ya kusimamia mitihani ya muhula uliopita ya wahadhiri wa Shule ya Sanaa na Sayansi za Jamii waliogoma na kukwamisha mitihani ya muhula huu iliyotakiwa kuanza mapema wiki hii.

Kaimu Mkuu wa Shule hiyo, Dk. Frowing Nyoni, alisema kuwa awali, hawakuwa na fedha za kulipa deni hilo, lakini wamehakikisha wanapambana mpaka fedha hizo zikapatikana.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanataaluma wa Chuo hicho (Udomasa), Mhadhiri Msaidizi Paulo Loisulie, na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Shule hiyo, Masatu Kyabwene, walithibitisha pande hizo mbili  kufikia suluhu na kwamba, mitihani iliendelea kama kawaida.

Hata hivyo, hivi karibuni kulielezwa kuwapo kuvurugwa mitihani mitatu, ambayo ilifanywa chini ya usimamizi wa wahadhiri, ambao siyo waliotakiwa kufanya kazi hiyo kufuatia waliostahili kuwa katika mgomo ambambo iliyotakiwa kufanywa na wanachuo wa mwaka wa tatu iligawiwa kwa wale wa mwaka wa kwanza, huku mtihani mmoja wa lugha (Literature) uliotakiwa kufanywa kwa kutumia vitabu wanachuo wakizuiliwa kutumia na hivyo kusababisha malalamiko.

Mhadhiri Msaidizi anayefundisha na aliyestahili kusimamia somo hilo, Honoratha Thomas, akizungumzia tatizo hilo  amesema wameafikiana mitihani yote mitatu iliyofanywa bila usimamizi wa wahusika isitambuliwe.

Hata hivyo, Dk. Nyoni alikataa kuzungumzia suala hilo akisema kwa kuwa bado wanalifanyia uchunguzi na kwamba ikibainika kulitokea matatizo, kuna hatua zinazotakiwa kufuatwa ili kuweka mambo sawa na kutaja hatua hizo kuwa ni pamoja na mitihani kurudiwa kutungwa upya au wanachuo kufanya katika muhula ujao kama mitihani maalumu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa