Home » » MAGHEMBE AWASILISHA NYARAKA ZA KUHUSU MNYIKA

MAGHEMBE AWASILISHA NYARAKA ZA KUHUSU MNYIKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe
 
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, amepokea barua kutoka kwa Katibu wa Bunge ikimjulisha kwamba Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, hatimaye amewasilisha nyaraka na ripoti za utekelezaji wa miradi ya maji katika Jiji la Dar es Salaam.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Katibu Msaidizi wa Mnyika, Aziz Himbuka, inasema kuwa taarifa hiyo imepelekwa katika Ofisi ya Mshauri Mkuu wa Mambo ya Sheria wa Bunge ili iweze kusomwa na hatua   zitakazohitajika zichukuliwe.

Alisema Mnyika ataanza kazi ya kuzipitia taarifa hizo  katika Ofisi Kuu ya Bunge Dodoma na baada ya kazi hiyo atarejea kuanza ziara ya kikazi jimboni kwake kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu 2014.

Mnyika anatarajia kufanya ziara katika kata zote 14, ambayo pamoja na mambo mengine atakagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ya maji.

Awali Mbunge huyo, alimtaka Waziri wa maji, taasisi, mamlaka na kampuni zilizo chini ya Wizara ya Maji kumpatia nakala ya nyaraka zinazohusu masuala ya maji katika Jiji la Dar es Salaam kwa kuzingatia masharti ya Sheria.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa