Home » » MSIGWA: WALIMU GOMENI MICHANGO YA LAZIMA

MSIGWA: WALIMU GOMENI MICHANGO YA LAZIMA

MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), amewataka walimu wa Halmashauri ya Manispaa Iringa, wagome kulipa michango ya lazima kwa ajili ya ujenzi wa maabara.
Msigwa, alitoa kauli hiyo mjini Dodoma juzi wakati akizungumza na Tanzania Daima.
Alisema amepata taarifa kutoka kwa baadhi ya walimu wa halmashauri ya Iringa, kwamba wamekuwa wakitishwa na kulazimishwa kulipa mchango wa sh 12,000 kwa ajili ujenzi wa maabara.
"Natoa wito kwa walimu Iringa, msikubali kulipa michango kwa lazima. Michango hiyo iwe kwa hiari na kama mtu hana, asitishwe, asilazimishwe," alisema Mchungaji Msigwa.
Mbunge huyo, alisema anatarajia kwenda Iringa kufanya mkutano na walimu wote na kuwapa elimu kutetea haki zao.
Alisema jukumu la kujenga shule na maabara zake ni la Serikali, lakini kwa vile haina mipango isitake kubebesha mzigo huo kwa walimu.
Walimu hao wanadai kuwa watendaji wa halmashauri ya manispaa ya Iringa mjini, wamekuwa wakiwatishia kwamba watakaogoma kuchangia kwa hiari, watahamishiwa vituo vya mbali.
Chanzo:Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa