Home » » DK. MAGUFULI: MAUAJI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YANANIUMIZA SANA, OLE WAO WATENDAJI WAZEMBE NITASHUGHULIKA NAO‏

DK. MAGUFULI: MAUAJI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YANANIUMIZA SANA, OLE WAO WATENDAJI WAZEMBE NITASHUGHULIKA NAO‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo akiendelea na kampeni zake za kuisaka Ikulu nchini Kote akiwaomba watanzania kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ili aweze kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.
Akitoa hotuba yake katika moja ya mikutano yake alioufanya katika mji wa Kibaigwa Dk. John Pombe Magufuli amesema hakuna kitu kinachomuumiza kama mauaji ya wakulima na wafugaji tanayotokea kati ya wilaya za Kongwa Mkoani Dodoma na Kiteto mkoani Manyara ni jambo ambalo linamuumiza sana kwani watanzania tumezoea amani na si mapigano.
Ameongeza kwamba katika serikali yake mara baada ya kuchaguliwa na kuunda serikali ni jambo ambalo ataliangalia kwa umiakini mkubwa. "Yaani Mimi Magufuli Nimteuwe Waziri na watendaji wengine wa serikali alafu Mauaji yatokee watu wafe. Mkuu wa mkoa yupo , Mkuu wa wilaya yupo na Kamanda wa Polisi yupo wabaki wanapunga upepo, wamiliki wa Ng'ombe wabaki wanakula maisha haiwezekani Nitalala nao mbele na Ng'ombe wataliwa msibani kwa uzembe waliosababisha"
Magufuli amewataka wafugaji na wakulima kuishi kwa amani bila kubaguana lakini pia akasema atatumia sheria za ardhi na kuhakikisha maeneo ya wafugaji na wakulima yanatengwa, ili wafanye shughuli zao na kukuza kipato na uchumi wao bila kusumbuliwa. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA)
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
???????????????????????????????????? ????????????????????????????????????
Umati wa wananchi ukiwa umefurika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kumsikiliza Dk. John Pombe Magufuli.
???????????????????????????????????? ????????????????????????????????????
Mzee John Samwel Malecela kulia akionyesha alama ya dole gumba kuashiria kukubali hotuba ya Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa akinyanyua kofia yake juu kuunga mkono.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi ilani ya Uchaguzi Mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini Mh. Anthony Mavunde.
????????????????????????????????????
Maonyesho ya mitindo ya mavazi pia yanaambatana na kampeni za uchaguzi kutokana na uvaaji wa wanawake mbalimbali wanaohudhuria katika mikutano ya kampeni kama huyu Mwanamama ambaye jina lake halikufahamika akiwa amejipigilia kilemba cha CCM na gauni lenye rangi za CCM njano na kijani nyuma likionekana bango la picha ya Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mzee Jaji Joseph Sinde Warioba akimpigia debe Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano huo mjini Dodoma.
????????????????????????????????????
Mzee John Samwel Malecela akimpigia debe Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli katika kutano huo uliofanyika mjini Dodoma.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa amekaa na viongozi mbalimbali na wastaafu kutoka kulia ni Jaji Joseph Warioba, Mzee John Samwel Malecela na Mwenyekiti wa CCM Dododma Alhaji Adam Kimbisa na kushoto ni Mgombea ubunge jimbo la Dodoma mjini Ndugu Anthony Mavunde.
????????????????????????????????????
Msanii Ali Kiba na kundi lake wakifanya vitu vyao jukwaani kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma katika mkutano wa kampeni wa Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Ali Kiba akiimbisha wananchi wakati akitoa burudani katika mkutano huo.
???????????????????????????????????? ????????????????????????????????????
Msanii Msami naye akafanya vitu vyake na kundi lake.
????????????????????????????????????
Vijana waleta vurugu wamedhibitiwa vyakutosha katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Jamhuri ikiwa imetapika.
????????????????????????????????????
Mh. Temba akikamua jukwaani.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Jamhuri tayari kwa kuhutubia mkutano huo wa kampeni.
???????????????????????????????????? ????????????????????????????????????
Vijana wakiwa wamevalia Ki- Father Christmass huku wakiwa wamejifunga vitambaa vya CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kibaigwa.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi ilani ya uchaguzi mgombea ubunge wa jimbo la Kongwa na aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Kibaigwa.
????????????????????????????????????
Akina mama wakifurahia hotuba ya Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli aliyoitoa kwenye mkutano wa kampeni Kibaigwa.
????????????????????????????????????
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mkutano huo uliofanyika mjini Kibaigwa wilaya ya Kongwa.
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa akimpigia debe Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Mzee Jaji Josepha Warioba wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Kibaigwa.
????????????????????????????????????
Wananchi hawa wakifuatilia kwa makini hotuba ya Dk. John Pombe Magufuli hayupo pichani wakati akiomba kura Kongwa mjini.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza mgombea ubunge wa jimbo la Kibakwe Mh. George Simbachawene wakati akiomba kura mjini Mpwapwa kwenye mkutano uliofanyika uwanja wa Mgambo kulia ni Mh. Rubeleje.
????????????????????????????????????
Wadau wangu Afande Mohamed Muhina wa Jeshi la polisi Mpwapwa na Juma Kengele kamanda wangu wakiwa katika mkutano huo uwanja wa Mgambo mjini Mpwapwa.
????????????????????????????????????
Bibi huyu akifurahia jambo huku akiwa ameshikilia picha ya Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya wananchi katika kijiji cha Mbande njiapanda ya Mpwapwa wakati aliposimamishwa ili asalimiane nao akiwa njiani kuelekea Mpwapwa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa