Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
Wauguzi
Wilayani Chamwino pamoja na wengineo nchini wamepewa pongezi kwa
mchango wao mkubwa wanaoutoa wa kutoa huduma ya afya kwa jamii ikiwemo
kuendeleza huduma hiyo nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mhe. George Lubeleje katika
Hospitali Teule ya Mvumi iliyopo Wilayani Chamwino mkoani Dodoma
wakati alipomwakilisha Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa
Tanzania, Mhe. Job Ndugai ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho
ya Siku ya Wauguzi Duniani.
Mhe.
Lubeleje amesema kuwa bila kuwepo kwa wauguzi huduma ya afya ingeyumba
kutokana na ukweli kwamba Wauguzi hao ni zaidi ya asilimia 60 ya
Watumishi wote wa sekta ya afya ambapo wanatekeleza asilimia 80 ya
shughuli zote za afya.
Amefafanua
kuwa, Wauguzi ndiyo wenye kuandaa mazingira mazuri kwa daktari
kutekeleza majukumu yake kwani baada ya daktari kumaliza kumuona mgonjwa
na kutoa maelekezo yake, muuguzi husimamia utekelezaji wa maelekezo
hayo pamoja na tiba na huduma kwa mgonjwa husika.
Ameongeza
kuwa, mara nyingi muuguzi ndiye anayefanya kazi ya kuuguza mgonjwa
kwani wagonjwa wengi hutumia muda mwingi wakiwa mikononi mwa wauguzi
kuliko wanaoutumia mikononi mwa wahudumua wengine wa sekta ya afya.
Aidha, Mhe. Lubeleji amewapongeza wauguzi hao kutokana na kaulimbiu yao katika Maadhimisho ya Wauguzi Duniani isemayo “Wauguzi; Nguvu ya Mabadiliko: Uboreshaji wa uthabiti wa mifiumo ya afya”
ambapo amesema kwamba ni kaulimbiu katika wakati muafaka kwakuwa
wauguzi wana nafasi maalum katika maendeleo ya huduma ya afya na sekta
yenyewe kwa ujumla.
“Ni
chachu muhimu ya mabadiliko katika sekta ya afya, na ndiyo rasilimali
ya kuwawezesha uboreshaji wa uthabiti wa mifumo ya afya”, alisema Mhe.
Lubeleje.
Akifafanua
baadhi ya changamoto zinazoikabili Hospitali Teule ya Mvumi wilayani
hapo, alisema kuwa Serikali inaelewa kuhusu mchango wa wauguzi na
inauthamini kwa kiasi kikubwa, vile vile amewahakikishia wauguzi hao
kuwa Serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha maslahi ya Watumishi wa Umma
wakiwemo wa afya, hususani katika masuala ya mishahara na posho
mbalimbali.
“Maombi
yenu nimeyapokea na ninaahidi nitayawasilisha kwenye Mamlaka husika kwa
ajili ya utekelezaji, yale yanayotuhusu, kama Bunge tutayachukua pia na
kuisimamia Serikali ili iyatekeleze na hatimaye tuimarishe huduma za
uuguzi na afya kwa ujumla”, alisema Mhe. Lubeleje.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Farida Mgomi amewasisitiza
Wauguzi wilayani hapo kujituma kwa bidii katika kutekeleza majukumu yao
ya kutoa huduma ya afya kwa jamii kwani Serikali ya Awamu ya Tano
inahitaji mabadiliko yanayoendana na kasi ya “Hapa Kazi tu” kwa
kuwahudumia wananchi nchini.
Aidha,
amewapongeza kwa juhudi zao na maarifa katika kazi yao na
kuwahakikishia kuwa Serikali itazidi kushirikiana nao katika kuleta
maendeleo katika sekta hiyo na kusimamia vema katika masuala yao
mbalimbali.
Sikua
ya Wauguzi Duniani huadhimishwa tarehe 12 Mei kila mwaka ikiwa ni
kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwanzilishi wa Uuguzi Bi. Florence Nightngale
aliyezaliwa tarehe 12 Mei, 1820 na kufariki mwaka 1910.
0 comments:
Post a Comment