SERIKALI
imewataka Mwenyekiti wa Serikali za Vijiji nchini kutangaza na kuweza
wazi taarifa za mapato na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo
katika kipindi cha kila baada ya miezi mitatu (3).
Hatua
ya kutotangaza taarifa hizo itaondoa uhalali wa mikutano mikuu
unaohitajika kuitishwa na Viongozi hao katika kipindi hicho, kama
inavyoelekezwa katika sheria ya fedha ya mamlaka ya Serikali za Mitaa ya
mwaka 1982.
Hayo
yamesemwa leo mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene wakati wa
mahojiano yake na waandishi wa habari waliotaka kufahamu umuhimu wa
wananchi wa vijijini kuifahamu bajeti ya Serikali.
Simbachawene
aliwataka Viongozi waliopo katika mamlaka ya Serikali za Mitaa wakiwemo
Madiwani kusimamia kikamilifu suala hilo ili kuhakikisha kuwa wananchi
waliowachagua wanafahamu matumizi ya fedha mbalimbali zinazotumwa na
Serikali katika Halmashauri za Wilaya.
“Wapo
baadhi ya Wenyeviti wamekuwa wakificha taarifa hizo kutokana na maamuzi
yasiyo ya busara katika matumizi ya rasilimali ikiwemo uuzaji wa ardhi,
hatua inayopelekea migogoro ambayo kimsingi haina umuhimu wowote”
alisema Simbachawene.
Kwa
mujibu wa Simbachawene alisema Mwenyeviti wa Mitaa, Vijijini na
Vitongoji hawana budi kutambua kuwa dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa
wananchi pamoja na mambo mengine inawahimizia viongozi hao kutoa taarifa
hizo katika kipindi kilichowekwa kwa mujibu wa sheria.
0 comments:
Post a Comment