Na. Immaculate Makilika- MAELEZO, Dodoma
Mstahiki Meya wa mji wa Dodoma Jaffari Mwanyemba, amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuwaenzi Mashujaa waliopigana katika vita mbalimbali ikiwa ni katika harakati za kuiletea uhuru nchi ya Tanzania.
Hayo yamesemwa leo saa sita usiku, wakati alipokuwa akizima Mwenge wa uhuru uliowashwa jana Julai 24, na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mheshimiwa
Christina Mndeme katika kilele cha mnara wa mashujaa mnano saa 6 kamili
usiku ikiwa ni sehemu ya maombolezo ya kumbukumbu ya Mashujaa,
yaliyofanyika katika Uwanja wa Mashujaa uliopo mjini Dodoma.
“Watanzania tuna jukumu la kuwaenzi Mashujaa kwa
kufanyakazi kwa bidii, nidhamu na uadilifu, na kama wote tutafanya
hivyo tutakuwa tumewaenzi mashujaa wetu” alisema Mstahiki Meya Mwanyemba
Ameongeza
kuwa kila mwananchi atimize uwajibu wake kwa kufanyakazi, ili kila
mmoja atapata haki yake na hivyo kuendelea kudumisha amani iliyopo
nchini.
Maadhimisho
ya kumbukumbu za Mashujaa kwa mwaka huu yamefanyika leo julai 25,
mkoani Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
0 comments:
Post a Comment