Na
Godfriend Mbuya
Naibu
Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Jinsia na Wazee na Watoto Dkt. Khamis
Kigwangalla amesema Serikali
itaendelea kutumia sheria zilizopo kwa ajili ya kutoa adhabu kwa wanaofanya
vitendo vya udhalilishaji kwa watoto pamoja na kutoa elimu kwa jamii lakini
siyo kuwahasi wanaume.
Dkt.
Kigwangalla amesema hayo bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa
Viti Maalumu CCM, Khadij Aboud aliyetaka kujua , pamoja na serikali kuwa sheria
nyingi lakini bado watoto wamezidi kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji, na
kuitaka serikali ieleze mkakati mbada wa kukabiliana na tatizo hilo.
'
Serikali itaendelea kutoa elimu pamoja na kufuata sheria ya mtoto ya mwaka 2009
na sheria nyingine za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
kukabiliana na matukio ya udhalilishaji wa watoto nchini” Amesema Dkt.
Kigwangalla.
Ameongeza
kuwa serikali haita wahasi wanaume wanaofanya vitendo hivyo badi itaendelea
kutoa elimu juu ya madhara ya udhalilishaji kwa watoto na kuitaka jamii iwe
mstari wa mbele katika kufichua na kukemea vitendo hivyo hususani kutoa
ushirikiano wa kutosha inapotokea kesi kama hizo.
“Familia
nyingi hazitoi ushirikiano wa kutosha kuhusu kesi za udhalilishaji wa watoto
nchini kwa kuhofia kumpoteza ndugu yao kutumikia kifungo jambo linalokwamisha
wahusika kupatikana na hatia kwa kukosa ushahidi wa kutosha” Amesema
Kigwangalla.
Aidha
Naibu Waziri amesema kuwa watoto ambao hufanyiwa vitendo hivyo husaidiwa kupata
usaidizi wa kisaikolojia kutoka kwa wataalamu waliopo vituo vya afya pa,moja na
ustawi wa jamii.
Wakati
huo huo akikazia majibu hayo Waziri mwenye dhamana ya afya nchini Ummy Mwalimu
amesema serikali ipo kwenye mchakato wa kuitaka mahakama,kutenga muda maalumu
wa kusikiliza kesi za watoto ili ziweze kushughulikiwa kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment