Home » » Mbowe ataka serikali isaidie wazazi wanaojenga mabweni

Mbowe ataka serikali isaidie wazazi wanaojenga mabweni


Na GODFRIEND MBUYA
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Haikaeli Mbowe ameiomba serikali mjini Dodoma itoe upendeleo kwa shule zote ambazo wazazi wamejitahidi na kuanzisha mabweni kwa ajili ya kidato cha tano na sita ili yaweze kukamilika.
Mbowe ameyasema hayo katika kipindi cha maswali na majibu bungeni, ambapo ameiomba serikali isaidie wazazi ambao wameonyesha nia ili shule hizo ziweze kufaidisha wengi.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jaffo amesema kutokana na umuhimu wa elimu na namna ambavyo baadhi ya wazazi wamejitoa ni lazima serikali itafanya linalowezekana kuweza kuwaunga mkono.
“Tutaweka kipaumbele katika eneo hilo na ushauri wako ni mzuri kwetu , na kweli kuna maeneo ambayo nimepita na kujionea na tunawapongeza wazazi wote wanaojenga mabweni ili wanafunzi wanaofaulu wasikose sehemu za kusomea na kulala” Amesema Jaffo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa