Judith
Mhina-Maelezo
Ushirikiano
wa Wazazi na Walimu –UWW wa Shule ya Msingi Uhuru Mkoa wa Dodoma, wamemkamata mwanafunzi
akiwa katika eneo la Bar ya Chako ni Chako jana Jumanne tarehe 25 saa 3 asubuhi.
Mwanafuzi huyo jina limehifadhiwa anasoma darasa la tatu ni mvulana ana umri wa
miaka11 alikutwa hapo muda wa masomo .
Hayo
yalisemwa na Mratibu wa Elimu wa Kata Uhuru Bibi Mary Rweikiza katika Manispaa ya
Dodoma. Akisimulia mkasa huo Bi Mary alisema, mmoja wa wazazi wa Ushirikiano wa
Wazazi na Walimu Bw Juma Hamisi alikuwa anapita katika eneo hilo na kumuona kijana
huyo akiwa anacheza hapo Bar na Watoto wanaishi katika mazingira magumu.
Aidha,
Mratibu Bibi Rweikiza ambaye ni mmoja wa washiriki wa semina ya Mawasiliano ya Mpango
wa Kuboresha na Kuinua Kiwango cha Ubora wa Elimu Tanzania EQUIP- Tanzania, ndio
chanzo cha uundwaji wa Ushirikiano wa Wazazi na Waalimu katika Mkoa mzima wa
Dodoma.
Bibi
Oliver Kapaya Mratibu wa Semina ya Mawasiliano ya Mpango wa Kuboresha na Kuinua
Ubora wa Elimu Tanzania alisema Ushirikiano huu wa Wazazi na Waalimu unaundwa baada
ya kuitisha kikao cha wazazi wa shule husika, wanachagua wazazi 2 wawakilishi kila
darasa kwa kuzingatia jinsia na mwalimu mmoja kila darasa,.
Baada
kuwapata wawakilishi hao wanachagua Mratibu wa umoja huo, kwa ujumla ushirikiano
huu unakuwa na wawakilishi 21., wazazi 14 kwa jinsia sawa na walimu 7.
Majukumu
ya Ushirikiano huo ni kusaidia kuimarisha ustawi wa wanafunzi shuleni, kudhibiti
utoro, kutoa taarifa au habari mbalimbali za shule kwa jamii husika na Taifa kwa
ujumla. Aidha, malengo ni kutatua migogoro baina ya shule yenyewe na jamii, kutoa ushauri na unasihi, kuthibiti nidhamu, na
kurejesha umakini kwa wanafuzi katika kupata elimu, kuweza kubaini aina za unyanyasaji shuleni na
kutafuta ufumbuzi wake. Na mwisho kusimamia shughuli za Klabu za wanafunzi,
michezo, ubunifu. Makambi ya masomo
Bibi
Kapaya aliongeza kwa kusema matokeo, ya Ushikiano huu umefanya wazazi kuelewa majukumu
yao kwa watoto, pia wazazi kuwa sehemu ya shule na katika kufanya maamuzi, kuboresha
mahusiano kati ya shule na jamii, kuboresha mahusiano kati ya shule na jamii,
kuinua kiwango cha ubora na ufaulu katika shule, kuboresha hali ya ustawi wa wananfunzi
ikiwa kuboresha afya zao na matumizi sahihi ya mazingira yanayowazunguka.
Mkoa
wa Dodoma una jumla ya shule za Msingi 727 ambapo kila shule ina wanafuzi kati ya
idadi ya juu 1,500 na ya chini 250 na shule zote hizo zina utendaji wa Ushirikiano wa Wazazi na Walimu – UWW.
0 comments:
Post a Comment