![]() |
Baadhi ya Viongozi
mbalimbali wa Serikali wakishuhudia uwashwaji wa Mwenge.
|
![]() |
Mwenge wa uhuru mara
baada ya kuwashwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh. Christina Mndeme, Tarehe
25 julai 2016 Saa Sita Kamili usiku Mkoani Dodoma.
PICHA NA HASSAN SILAYO |
Na. Immaculate Makilika Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama amesema kuwa kufanyika
kwa maombolezo ya kumbukumbu za Mashujaa inawakumbusha watanzania kuwa
wazalendo.
Akizungumza wakati wa maombolezo ya kumbukumbu za Mashujaa
sambamba na kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru katika mnara wa kumbukumbu za Mashujaa,
leo usiku katika viwanja wa Mashujaa vilivyopo
mjini Dodoma, Waziri Mhagama alisema
kuwa kufanyika kwa maombolezo ya Mashujaa mkoani Dodoma ni heshima kwa wananchi
wa Dodoma na watanzania wote kwa ujumla.
“Kufanyika kwa maombolezo haya inatukumbusha watanzania kuwa wazalendo na
kupigania bila kuchoka, bila kujali makabila yetu na tujifunze kwa Mashujaa
hawa waliopigania uhuru wetu” alisema Waziri Mhagama.
Waziri Mhagama aliwaomba watanzania kutumia siku ya kumbukumbu ya Mashujaa ambayo
ni Julai 25, kwa namna mbalimbali ikiwemo kufanya maombi ya sala kwa Mashujaa wote walifariki katika
harakati mbalimbali za kupigania uhuru wa Taifa la Tanzania.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimwa Jordan
Rugimbana aliishukuru Serikali kwa uwamuzi wa kuadhimisha kumbukumbu za mwaka huu za Mashujaa mkoani Dodoma, na
kusema kuwa kufanyika kwa tukio hilo la kihistoria linakumbusha uwajibu wa
watanzania na Mkoa wa Dodoma utaienzi heshima hiyo.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mheshimiwa Christina Mndeme
aliwasha Mwenge wa Uhuru katika kilele cha mnara wa mashujaa mnano saa 6 kamili
usiku ikiwa ni sehemu ya maombolezo ya
kumbukumbu ya Mashujaa.
Mnara wa Mashujaa uliopo mkoani Dodoma ni kati ya vituo 4
vilivyopo nchi nzima ambavyo vimekuwa na makaburi ya Mashujaa mbalimbali
waliopigania uhuru wa nchi ya Tanzania. Vituo vingine vipo meneo ya Mtwara, Dar
es Salaam na Kagera.
Maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa kwa mwaka huu
yanatarajiwa kufanyika kesho julai 25, mkoni Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi.
0 comments:
Post a Comment