Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Siku chache baada ya wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba (Ukawa)
kutoka bungeni, Pamela Maasay amesema hana hofu ya kufukuzwa ujumbe wa
Bunge hilo kwa sababu ya kutetea kazi iliyompeleka bungeni.
Maasay alikuwa akizungumzia maoni ya baadhi ya
wajumbe, yaliyotaka waondolewa kwenye Bunge hilo kutokana na hatua
waliyochukua. “Kuna maombi yametolewa yakitaka wajumbe tulioteuliwa na
Rais (wale 201) tuliotoka bungeni tuvuliwe ujumbe, kimsingi sina hofu ya
kuondolewa ndani ya hilo Bunge kwa sababu nasimamia Rasimu ya Katiba
ambayo niliteuliwa kuifanyi kazi,”alisema.
Alisema kushiriki mijadala isiyo zingatia msimamo
wa wananchi, ni kushiriki kunyima haki Watanzania na kutokuitendea haki
kampuni yake ambayo kutokuwapo kwake kazini, inapoteza fedha.
Maasay anayetoka kundi la wajumbe wateule 201,
alisema kutokuwepo kazini, mwajiri wake kampuni ya CocaCola Kwanza,
inapoteza Sh400 milioni. Alise sababu ya kuungana na waliosusia Bunge ni
kwa kuwa amegundua hakuna nia wala dhamira ya dhati ya kufanya
kilichowapeleka.
“Bunge limekuwa la majigambo na mashairi, kila
anayesimama kuchangia mjadala hajadili rasimu bali yale anayojisikia
kueleza, kana kwamba hakuna kanuni,” alisema.
Alisema baada ya mwenendo wa Bunge kwenda kinyume
na matarajio, CCM walipaswa kuwa wa kwanza kusitisha mchakato wa Katiba.
Alibainisha kuwa hakuunga mkono kutoka nje ya Bunge hilo kwa sababu
waliyofanya hivyo ni Ukawa, angefanya hivyo kwa kundi lolote.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment