Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Endtime Havest, Dk Elia Mauza amewataka
viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutorudi katika Bunge
Maalum la Katiba hadi maoni ya wananchi yatakapoheshimiwa.
Akizungumza na Tanzania Daima jana muda mfupi baada ya kumalizika kwa
ibada ya Jumaapili, Askofu Dk. Mauza ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Umoja
wa Madhehebu ya Kikristo Mkoa wa Dodoma, alisema kitendo cha viongozi
kutokuwa waaminifu katika kujadili rasimu ya katiba ni kutowatendea haki
Watanzania.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment