Home » » TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: WAZIRI MKUU MTEULE KUAPISHWA KESHO NOVEMBA 20,2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: WAZIRI MKUU MTEULE KUAPISHWA KESHO NOVEMBA 20,2015

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


YAH: SHEREHE ZA KUMUAPISHA WAZIRI MKUU MTEULE

Sherehe za kumuapisha Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa,  Waziri Mkuu Mteule zitafanyika katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Novemba, 2015 kuanzia saa   4.00 Asubuhi.

Sherehe hizo zinafanyika siku moja  baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha jina lake kwa kura nyingi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia uteuzi uliofanywa na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba ya sherehe hizo, Wageni waalikwa wote wanapaswa kuwasili katika Ikulu ya Chamwino kuanzia majira ya saa mbili asubuhi.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo  Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu wastaafu na waheshimiwa wabunge.

Imetolewa na Idara ya Habari MAELEZO
19 Novemba, 2015
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa