Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na
Lilian Lundo
Maelezo
Dodoma
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania wamemchagua Mhe.Dkt. Tulia Akson kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)
kuwa Naibu Spika wa Bunge la 11 baada ya kumshinda mpinzani wake kutoka Chama
cha Wananchi (CUF) Mhe. Magdalena Sakaya.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mhe. Dkt.
Akson kushinda kwa kura 250 ambazo ni
sawa na asilimia 71.2 za kula halali dhidi ya mpinzani wake Mhe. Sakaya
aliyepata kura 101 ambazo ni sawa na asilimia 28.8 ya kura halali.
Uchaguzi huo umefanyika leo, Mjini
Dodoma ambao ulitanguliwa na uthibitisho wa jina la Waziri Mkuu Mheshimiwa
Kassim Majaliwa.
Akiomba kura kwa wabunge Mhe. Dkt. Akson
alisema kuwa atajitahidi kuwatunukia
wananchi wote bila kujali tofauti za kisiasa ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Aliongeza kuwa atajitadi kumshauri vizuri Spika juu ya Sheria na Kanuni kwa
kutumia uzoefu alionao kama Mwanasheria mzoefu ili kuhakikisha haki
inatendeka kwa wote.
Akimpongeza Mhe. Dkt. Akson Tulia kwa ushindi alioupata,
Mhe. Sakaya alisema kuwa matarajio yake
na watanzania ni kuona nchi inakuwa na
Bunge imara litakalo fanya kazi zake kwa uimara bila ubaguzi ili kuiletea nchi
maendeleo.
Akitoa neno la shukurani mara baadaya
kuchaguliwa Mhe. Dkt. Akson alimshukuru Mhe. Rais kwa uteuzi alioufanya
wa kumteua kuwa Mbunge na hatimaye kugombea nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la
11.
“Naahidi nitawatumikia kama mtumishi
wenu, tutafanya kazi kiufanisi na pia
nitatumia weledi wangu katika kazi zangu kama Naibu Spika, naomba msisite
kuniletea hoja zenu pale mnapokuwa nazo,” alisema Mhe. Dkt . Akson.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa Naibu Spika
Mhe. Dkt. Akson alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali .
0 comments:
Post a Comment