Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
Dodoma
19.11.2015
WAZIRI
Mkuu mteule wa Serikali ya Awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amesema
hakutegemea nafasi ya jina lake kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kshika wadhifa wa nafasi hiyo kubwa katika Serikali.
Alisema
Uteuzi huo ulioidhinishwa na Bunge, umedhihirisha imani ya Rais Dkt. John Pombe
Magufuli aliyonayo kwake iliyomwongoza katika kuliwasilisha jina lake Bungeni.
Akizungumza
mara baada ya zoezi la uthibitisho wa uteuzi wa jina lake Bungeni Mjini Dodoma
(leo), Mhe. Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa alisema kilichopo mbele
yake kwa sasa ni kuwatumia Watanzania pasipo kujali itikadi ya vyama vyao.
Aliongeza
kuwa mara baada ya kuanza kazi yake atahakikisha anazunguka katika mikoa mbalimbali
nchini ili kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania na maendeleo
yaliyofikiwa katika sehemu mbalimbali.
Aidha
Mhe. Majaliwa aliwahakikishia Wabunge ushirikiano wa karibu zaidi katika
kupokea ushirikiano ili kuweza kuwaletea maendeleo ya haraka Watanzania.
Awali
akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa na Wabunge wa Bunge kwa ajili ya
kuidhinisha jina hilo, Msimamizi wa jina hilo ambaye ni Katibu wa Bunge, Thomas
Kashilill ah alisema katika uchaguzi huo, Mhe. Majaliwa alipata kura za Ndiyo
258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote.
Aidha
Kashilillah alisema kura 91 sawa na asilimia 25% ya kura zote zilisema hapana
wakati kura 2 sawa na asilimia 0.06% ya kura zote ziliharibika.
Wakizungumzia
uteuzi huo, Wabunge mbalimbali Bunge la Jamhuri ya wamesifu uteuzi waMhe.
Kassimu Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa kusema ni kiongozi mwadilifu,
mchapakazi na asiye na makundi.
Wakizungumza
kwa wakati tofauti mjini hapa katika mkutano wa Bunge mjini Dodoma, wabunge hao
walisema, walisema uteuzi wa Mhe. Majaliwa ni chaguo sahihi katika Serikali ya
Awamu ya Tano ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuzingatia kauli ya hapa kazi tu.
Mbunge
wa Ismani (CCM), Mhe. Wiliam Lukuvi alisema uteuzi huo umekuja katika wakati mwafaka kwa
kuzingatia kuwa Mhe. Majaliwa amepata
uzoefu wa kutosha katika katika Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI hivyo anao uelewa
wa kutosha kuhusu matatizo mbalimbali ya nchi yetu ikiwemo sekta ya Elimu.
“Mhe.
Majaliwa ni Mwalimu na mara zote Walimu ni watu wa kujifunza, amekuwa Naibu
Waziri TAMISEMI kwa muda mrefu, amejibu maswali mbalimbali Bungeni yanayoihusu
TAMISEMI na pia amezunguka katika maeneo mbalimbaliya nchi na kujinea matatizo
ya Watanzania, hivyo ni chaguo sahihi”
Naye
Mbunge wa Newala Mjini (CCM), Mhe. George Mkuchika alisema Mhe. Rais amaengalia
vizuri kuhusu uteuzi wa Mhe. Majaliwa kwani, Mhe. Majaliwa ni kiongozi
mwadilifu, mchapakazi na pia ni mmoja wa Viongozi aliyekuwa na ushirikiano na uhusiano wa karibu na
Wabungewote wa Bunge lililopita, na hivyo ana imani kuwa uteuzi wakeutalisaidia
Bunge katika kujenga umoja na mshikamano.
Aidha
Mbunge wa Kaliua (CUF), Mhe. MagnalEna Sakaya alisema anamfahamu Mhe. Majaliwa
kwa kipindi kirefu kama Kiongozi mchapakazi na aliye tayari kujishusha na kuwatumikia wananchi wote pindi kujali
itikadi za vyama vya siasa.
“Namfahamu
vizuri sana Mhe.Majaliwa kuliko mtu yeyote kwani amekuwa Mkuu wa Wilaya ya
Urambo kwa kipindi cha miaka 5, ambapo alifanya kazi zake kwa ushirikiano
mkubwa zaidi na wananchi, hivyo kuteliwa kwake kuwa Waziri Mkuu kutalisaidia Bunge na Serikali.”
Mhe.
Sakaya alisema , anaunga mkono uteuzi wa Mhe. Majaliwa kwani ni kiongozi asiye
na chembe ya ufisadi na iwapo Serikali ingewasilisha jina la Kiongozi mwenye
kashfa, wabunge wa kambi ya upinzani wangeungana pamoja kupinga uteuzi wa
kiongozi huyo.
Mbunge
wa Msalala (CCM),Mhe. Ezekiel Maige alisema Mhe. Rais Joseph Magufuli amemteua
mtu sahihi katika nafasi ya Waziri Mkuu, kwani kwa uzoefu alionao ikiwemo
nafasi ya Naibu Waziri wa TAMISEMI na Mkuuwa Wilaya utaweza kumsaidia kusimamia
shughuli mbalimbali za Serikali ndani ya Bunge.
Mhe.Maige
alisema Mhe. Majaliwa ni miongoni mwa Viongozi walio mstari wa mbele katika
ulinzi na uhifadhi wa rasilimali za Taifa ikiwemo mapambano dhidi ya uharibifu
wa mazingira “kuna wakati Fulani wakati ule akiwa Mkuuwa Wilaya alikoswakoswa
msituni kutekwa na majangili wakati
alipoongoza operesheni ya kuzuia
majangili, hivyo ni kiongozi sahihi” alisema Mhe. Maige.
Mbunge
wa Momba Mhe. Job Silinde alisema uteuzi wa Mhe. Majaliwa ni chaguo sahihi,
kwani ni mtu aliye tayari kujishusha na
kuwa karibu na watu wote pasipo na kujali itikadi ya vyama vya siasa, na hivyo
Wabunge wote hawana budi kutoa ushirikiano kwake ili aweze kutekeleza vyema
majukumu yake.
“Mhe.
Majaliwa amekaa TAMISEMI, na Ofisi ile ni Mhimili wa nchi, hivyo amepata uzoefu
wa kutosha kuhusu nini maana ya Serikali na namna inavyoendesha kazi zake na
umri alionao ni umri wa kati na ataweza kuendana na kasi ya Serikali
itakayoundwa na Mhe. Rais John Pombe Magufuli.” Alisema Mhe. Silinde.
Mhe.
Silinde alisema wakati akiwa TAMISEMI, Mhe. Majaliwa alikuwa Naibu Waziri na
kuwa chini ya Viongozi wake, Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Mizengo Pinda na Waziri
wa TAMISEMI Mhe. Hawa Ghasia, hivyo kupitia Viongozi hao amejifunza masuala
mbalimbali ya Serikali ikiwemo usimamizi wa shughuli za Serikali Bungeni.
0 comments:
Post a Comment