Home » » Bunge limemuangusha Rais Magufuli-Mtatiro

Bunge limemuangusha Rais Magufuli-Mtatiro

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mwanasheria kutoka Chama cha Wananchi CUF Julius Mtatiro amesema Bunge limemwangusha Rais Magufuli  kwa kuchagua kamati dhaifu katika kamati zilizotangazwa hivi karibuni.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mtatiro amesema kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) imewekwa wabunge wageni kutoka upinzani na kamati hiyo inatakiwa kuongozwa na Mbunge kutoka upinzani hivyo lengo hapa la kuisimamia serikali halijapewa kipaumbele.

''Rais Magufuli alipolihutubia bunge aliomba kupewa ushirikiano wa hali ya juu kuchagua wabunge wapya wa kusimamia hesabu za serikali ni kuwapa wabunge hao mzigo mzito, kamati hii ilikuwa ikiongozwa na Zitto na serikali iliona uwezo wake ndiyo maana wametafuta watu ambao hawana uzoefu jambo ambalo sii zuri''Amesisitiza Mtatiro.

Mtatiro ameongeza kuwa ''Spika Ndugai hakuhitaji elimu ya Chuo Kikuu katika kufanya uteuzi wa kamati hizi na sidhani kama kuchaguz kamati dhaifu kama hizi hakuashiriii dhana ya Rais Magufuli ya hapa kazi tuu''.

Kuhusu Tume ya uchaguzi Zanzibar kutangaza tarehe ya uchaguzi Mtatiro amesema kilichofanyika Zanzibar ni makusudi matupu na kama CUF haitashiriki katika uchaguzi huo ni wazi kuwa kutakuwa na sintofahamu kisiwani humo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa