Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri 
 wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), 
George Simbachawene amesema atahakikisha shule zote hapa nchini zinakuwa
 na madawati yanayofanana.
Alisema
 hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari kuzungumzia 
changamoto za elimu bila malipo iliyoanza kutolewa Januari mwaka huu.
“Katika
 historia ninayotaka kuandika ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa 
chini katika kipindi cha miaka miwili lazima tuondokane na tatizo hili,” alisema na kuongeza kuwa atakuja na ubunifu utakaoondoka tatizo hilo nchini.
“Nataka
 kuwe na madawati yanayofanana nchi nzima yenye lebo ya For Government 
Primary School, ninaona mwanga mkubwa mbele yangu na katika hili 
ninaweza kufanikiwa nipeni fursa,” alisema.
Alisema
 pia kumekuwa na changamoto kubwa ya matumizi ya fedha zilizopelekwa kwa
 ajili ya kugharamia elimu na kuongeza lengo la serikali kutoa elimu 
bila malipo litabaki pale pale kwani miaka ya nyuma watoto wengi 
walishindwa kupata elimu kutokana na gharama kuwa kikwazo kwao.
Simbachawene
 alisema changamoto kubwa ni kwa walimu kudhani fedha zilizopelekwa 
shuleni ni za mwaka mzima lakini ukweli ni kuwa fedha ni za kila mwezi.
Alisema
 kila mwanafunzi wa shule ya msingi ya serikali atatoa shilingi 10,000 
na kwa sekondari ni shilingi 25,000 kwa mwaka kwa ajili ya uendeshaji wa
 shule.
Waziri
 huyo alisema kwa shule za sekondari za kutwa kila mwanafunzi atapata 
shilingi 3,540 na kwa shule ya sekondari ya bweni ni shilingi 7,243.
“Ukiwa
 na wanafunzi 500 maana yake shule inapata zaidi ya shilingi milioni 3.6
 kwa mwezi mmoja tu je ukipata fedha hizo unashindwa kuendesha shule?” alisema
 na kuongeza kuwa serikali pia ilipeleka fedha za chakula ili watoto 
waweze kula lakini fedha hizo zisitumike kulipa madeni ya samani ya 
wazabuni.
Aliwataka walimu wasivunje moyo juhudi zinazofanywa na serikali kwani mzazi masikini amepokea mzigo mzito sana na serikali.
“Tutakapokuja
 kwenye bajeti ya kwanza ya awamu ya tano tutakuwa tumejifunza 
changamoto. Tutaboresha na mambo mengine mazuri yatakuja,” alisema.
KIJUKUU CHA BIBI K BLOG 

0 comments:
Post a Comment