Home » » Waziri Lukuvi awaandikia wabunge wote barua.

Waziri Lukuvi awaandikia wabunge wote barua.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh.William Lukuvi,amewaandikia wabunge wote barua akiwataka waeleze migogoro ya ardhi iliyopo katika majimbo yao.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Babati Mjini Cecilia Pareso (CHADEMA) aliyetaka kujua hatua za serikali katika kutatua migogoro ya ardhi baina ya wananchi wake na hifadhi ya mbuga za wanyama Tarangire.

''Mheshimiwa Spika mimi nimewaandikia wabunge wote barua na nikiwataka kila mmoja anieleze katika eneo lake mgogorowa ardhi uliopo iwe ni kati ya vijiji na hifadhi ,misitu,au na wawekezaji ili iwe rahisi kwangu kuishughulikia''.Amesisitiza Lukuvi

Aidha Lukuvi ameongeza kuwa seikali ya awamu ya tano imejipanga vyema katika kutatua kabisa matatizo ya migogoro ya mara kwa mara ya ardhi hapa nchini

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa