Home » » NEWS ALERT: WABUNGE AMBAO WATAIWASILISHA TANZANIA HAWA HAPA

NEWS ALERT: WABUNGE AMBAO WATAIWASILISHA TANZANIA HAWA HAPA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Leo bunge limefanya uchaguzi wa wabunge watakaosimamia taasisi ya bunge pamoja na wabunge ambao wataiwakilisha Tanzania katika nchi washirika wa maendeleo.

Ambao wamechaguliwa katika tume ya utumishi wa bunge ni pamoja na Kangi Lugola,Mussa Zungu,Fakhari Shomari Khamis,Mary Chatanda,Salim Hassan Mtuki na upande wa upinzani utawakilishwa na Magdalena Sakaya pamoja na Mchungaji Peter Msigwa.

Bunge la Afrika litakuwa na uwakilishi wa wabunge wafuatao Mboni Mhita,Asha Abdula Juma,Dkt. Faustine Ndugulile,Steven Masele na upande wa upinzani utawakilishwa na David Silinde.

Jukwaa la wabunge kusini mwa Afrika (SADC) ni pamoja na wafuatao Jamal Kassim Ali,Ester Michael Mmasi,Selemani Jumanne Zedi,Ali Sale Ali, na Magreth Sitta.

Kwa upande wa Bunge la jumuia ya madola Tanzania itawakilishwa na Amina Mollel,Maria Kangoye,Zainabu Vulu,Khamis Mtumwa Ali,Salim Rhehani,Jitu Soni,Josephat Kandege, Immaculate, Raphael Chegeni,Juma Omari na Tundu Lissu.

Aidha umoja wa mabunge duniani Tanzania itawakilishwa na Pudensiana Kikwembe,Mohamed Chengella,Peter Serukamba, Juma Othman na Susan Lyimo.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa