Serikali imesema inajipanga kuandaa
mchakato mzuri utakaotumika katika kutoa pensheni kwa wazee wote hapa
nchini ili kuheshimu mchango wao katika kuitumikia jamii.
Serikali imeyasema hayo Bungeni Mjini
Dodoma ambapo Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira Anthon
Mavunde amesema ni dhamira ya serikali na ni ahadi ya Rais Dkt John
Magufuli na pia ni ilani ya chama cha Mapinduzi kwamba pensheni
itatolewa kwa wazee ili kuheshimu mchango wao.
Majibu ya Serikali yametokana na swali
ambalo ameuliza Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche (CHADEMA) aliyetaka
kujua ni kwanini serikali haiheshimu mchango wa wazee ambao
wamelitumikia taifa hili kwa muda mrefu na hawapati chochote huku
serikali ikiendelea kutoa ahadi zisizotekelezeka.
Aidha Naibu Waziri Anthon Mavunde
amewahakikishia wazee kwamba ahadi ya Rais ipo pale pale ila wavute
subra ili serikali ipate nafasi ya kujipanga vizuri ili kuweza kuhimili
wazee wote bila ubaguzi wowote.
0 comments:
Post a Comment