Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Yussuf Massauni
akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika kikao cha 7 cha Bunge la
11 linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi imejipanga kudhibiti uhalifu
unaofanywa na na baadhi watu kwa kupora fedha za wafanyabiashara au
watu binafsi kwa kutumia usafiri wa Pikipiki maarufu kama bodaboda.
Akijibu swali la
Mhe. Oscar Rwegasira Mukasa Mbunge wa Biharamulo Magharibi (CCM)
lililouliza ni zipi takwimu sahihi za matukio ya ujambazi yanayohusiana
na uporajiwa fedha,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad
Yussuf Massauni amesema matukio ya ujambazi yanayohusisha uporaji wa
fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015 kama takwimu
zinavyosema , kwa mwaka 2013 matukio 1.266, mwaka 2104 matukio 1,127 na
mwaka 2015 yalikuwa 931.
”
Jeshi la polisi limechukua hatua kwa kufanya kazi karibu na mabenki
nchini ili kubaini kama kuna wafanyakazi wa mabenki wanashirikia na
majambazi kufanya uporaji huo na watakaobainika tutawachukulia hatua
kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani
watakaokamatwa”
“
Napenda kuwaomba wananchi kutupa ushirikiano na hasa kwa
wafanyabiashara wanaochukua fedha nyingi ili tuweze kuwapatia ulinzi ili
kupunguza, ama kuondoa kabisa vitendo hivi vya uporaji wa fedha
vilivyokothiri nchini kwa sasa” Alisema Mhe Massauni.
Aidha amewaomba
waheshimiwa Wabunge kutoa elimu kwa wananchi wao kuhusu maswala ya
ulinzi na usalama ili kupunguza vitendo vya uhalifu hasa uporaji wa
fedha kwa wafanyabiashara kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wakiona
tukio lolote linalopangwa kwa ajili ya kupora fedha.
Serikali kupitia
Jeshi la Polisi linafanya ukaguzi wa pikipiki zote nchini ili kubaini
uhalali wake na uhalali wa wamiliki wake ili kuweza kubaini pikipiki na
wamiliki wanaohusika na vitendo vya uporaji wa fedha vinavyoshamiri siku
hadi siku
0 comments:
Post a Comment