SERIKALI imesema itaendelea kuvitambua vyeti vya wanafunzi
waliomaliza na kupangiwa madaraja katika mfumo wa GPA licha ya kurudi
katika mfumo wa divisheni kwa sasa.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ambaye alikiri kuwepo
changamoto nyingi ambazo hutokea kulingana na mahitaji ya wakati husika
na maoni ya wadau.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara
(Chadema), Profesa Ndalichako alisema mpango wa Serikali ni kupokea
maoni kutoka kwa wanajamii kulingana na mahitaji ya wakati huo na mfumo
wa marekebisho nayo hufanywa kulingana na nyakati.
Katika swali lake la msingi, Waitara alitaka kujua lini Serikali
itapeleka bungeni marekebisho ya sheria ya NECTA kwenye kifungu hicho
ili kuondoa nguvu ya waziri kutoa maelekezo bila kuhoji wala
kushirikisha wataalamu wa elimu.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella
Manyanya, alisema kifungu hicho kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya
elimu kufanya maamuzi kwa niaba ya Serikali pale inapolazimu.
Alisema maamuzi hayo huzingatia wakati, mazingira halisi na matokeo
ya tafiti mbalimbali kutoka kwa wataalamu pamoja na maoni ya wadau wa
elimu ambapo Baraza la Mitihani hutakiwa kuyatekeleza.
“Serikali kwa sasa haina mpango wa kukifanyia marekebisho kifungu
hicho cha Baraza kwa kuwa kinamwezesha waziri kutekeleza mahitaji ya
wakati huo.
Chanzo Gazeti la Mtanzania
0 comments:
Post a Comment