Home » » ‘TBC MKARABATI NYUMBA MLIZOTELEKEZA’

‘TBC MKARABATI NYUMBA MLIZOTELEKEZA’

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, ameagiza Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kuhakikisha nyumba zilizotelekezwa na shirika hilo kwa zaidi ya miaka 20 zinakarabatiwa haraka iwezekanavyo.
Akizungumza wakati wa kupata mrejesho wa maagizo aliyoyatoa kwenye ziara yake ya kwanza ya kukagua mali za TBC, Aprili 9 mwaka huu, Wambura alisema ni vyema kumalizia ujenzi wa nyumba hizo ambazo awali zilikuwa ndani ya pori.
Katika ziara yake ya kwanza, Wambura aliitaka TBC kuhakikisha inafanyia usafi eneo hilo ambalo lilikuwa pori na kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha wanapata hati ya kiwanja hicho.
“Mimi sitakubali kuona rasilimali kama hii inapotea na kuharibika bure wakati ni kodi za wananchi, sasa muamue kama mnataka kuendeleza eneo hilo basi muliweke kwenye mpango wa kulitekeleza haraka sana,” alisema.
Alisema andapo TBC itaona hawawezi kuliendeleza eneo hilo basi walipeleke Halmashauri ili wananchi walitumie kama mabweni ya wanafunzi kama ambavyo diwani wa kata ya Kisarawe alivyoomba.
“Ukiangalia ni majengo imara na uwekezaji wake unaonekana ulitumia fedha nyingi, kwani kutokana na kuwa magofu kwa zaidi ya miaka 20, lakini nyumba hizi (ziko hatua ya linta) hazina nyufa ingawa kuna nondo zimeibiwa,” alisema.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TBC, Joselin Lugola alisema uamuzi wa kuendeleza eneo hilo au la litajadiliwa kwenye menejimenti.
“Tutalijadili kwenye manejimenti. Tunachofanya sasa ni kuwaomba Wakala wa Majengo (TBA) kutufanyia tathimini ya gharama baada ya hapo tutajua nini cha kufanya ili tuingize kwenye bajeti ya mwaka 2017/18,” alisema.
Alisema TBC imekuwa ikiweka mipango ya kukarabati katika majengo katika maeneo mengi, lakini inakwama kutokana na ufinyu wa bajeti huku akisisitiza kuwa bajeti ijayo wamepanga kukarabati majengo ya Mwanza, Arusha na Dodoma.
Kuhusu hati ya kiwanja chenye meta za mraba 9,567 kilipimwa na kusajiliwa kwa namba 68,480 mwaka 2012, Wambura alipongeza hatua iliyofikia ya kupelekwa maombi ya hati kwa Kamshina ya ardha kanda ya Mashariki iliyopo Morogoro.
Awali, Ofisa Ardhi, Cheyo Nkelege alikiri ofisi yake kukosea kutoa fomu iliyokuwa ina sehemu ya kusaini mtu mmoja badala ya watu wawili kama inavyotakiwa kwenye fomu za taasisi au kampuni.
Fomu za awali zilikuwa na eneo moja la kusaini na zilisainiwa na Meneja Rasilimali Watu, Neema Mrindoko ikiwa ni kinyume na taratibu za fomu za umiliki wa ardhi wa taasisi au kampuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoko alisema kwa kushirikiana na TBC wamerekebisha makosa ya awali na kuwa fomu hizo zimeshapelekwa kwa kamishna wa ardhi. Alisema muda wowote shirika litakabidhiwa hati ya umiliki wa kiwanja hicho.

Chanzo Gazeti la Habari leo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa