Home » » BANGI EKARI 10 ZATEKETEZWA

BANGI EKARI 10 ZATEKETEZWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Imeandikwa na Lubasi, Mpwapwa
KATIKA kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imeweza kuteketeza ekari 10 za mashamba ya bangi huku watuhumiwa 34 walipatikana na dawa za kulevya aina ya bangi
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri, wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya zilizo katika mapambano ya dawa za kulevya, ambapo katika kipindi cha Januari hadi Juni 2017, wilaya hiyo iliweza kuteketeza mashamba ya bangi yenye ukubwa wa ekari 10 katika maeneo matatu tofauti.
Pia alisema kwa nyakati tofauti, jumla ya watuhumiwa 34 walikamatwa baada ya kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi. Alisema kati ya watuhumiwa waliokamatwa, 16 walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo kati ya mwaka moja hadi miaka 30 pamoja na kulipa faini.
Pia alisema bangi iliyokamatwa ni gunia moja, kilo moja na gramu 542, misokoto tisa na kete 121. Shekimweri alisema wilaya inaendelea kutoa elimu kwa vijana wasijiingize katika matumizi ya dawa za kulevya ambapo pia wilaya imeanzisha kikundi cha vijana cha waliokuwa wanatumia dawa hizo ili waweze kuwaelimisha wenzao madhara ya dawa hizo na kuziepuka.
CHANZO HABARI LEO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa