Home » » Mh. Spika akubali kuwasilishwa kwa hoja ya wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imauni na Waziri Mkuu siku ya jumatatu

Mh. Spika akubali kuwasilishwa kwa hoja ya wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imauni na Waziri Mkuu siku ya jumatatu


Muda mfupi kabla ya kumalizika kikao Cha Bunge jioni ya leo mjini Dodoma,Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu alisimama kutaka muongozo wa Spika kuhusu Suala linaloendelea kwenye Bunge hilo la kukusanya Saini za wabunge wapatao 70 ili kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mh. Lissu alisema kuwa kitendo cha Spika kutoa uamuzi kwa jambo ambalo halijamfikia mezani kwake ni kama ukiukwaji wa kanuni na sheria za Bunge na itaonyesha kuwa kuna majibu yanaandaliwa kwa hoja ambayo hatakuiona bado hajaiona na kwa kufanya hivyo nikukiuka taratibu.

Baada ya Mh.Lissu kutaka muongozo huo,Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda alisema kuwa hajasema kwamba suala hilo si halali kufanyika ila alichosema halitawezekana kwa kikao hiki cha Bunge,kwa sababu linamalizika siku ya Jumatatu (23 April,2012), kwahiyo itakuwa ni vigumu sana kulifanya jambo hilo ndani ya Kikao cha Bunge hili.

Aidha akitoa ufafanuzi zaidi Mh. Spika mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Mh. John Mnyika,kusimama na yeye akitaka muongozo juu ya jambo hilo hilo ambapo alihoji kwamba,kuna tatizo gani kama watu wakiendelea kusaini (saini ambazo Mh. Mnyika alisema idadi yake imefikia 66 ) na kuwasilisha hoja siku ya jumatatu kwaajili ya kujadiliwa Bunge lijalo?


Mh. Anne Makinda alisema kwamba yeye hajasema kwamba jambo hilo halifai, "Naomba nieleweke na answered zitaletwa,sasa hivi nilicho kisema! nikwamba suala hilo haliwezekani kwa Bunge hili kwakuwa jumatatu ndio linafikia kikomo lakini kama mtaleta kwa kikao kijacho hakuna tatizo" alisema Makinda. 
Habari kwa hisani ya Michuzi Blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa