mkurugenzi mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka akiwasilisha mada kwa wastaafu wa mkoa wa Dodoma
Katibu mkuu chama cha wastaafu mkoani dodoma bw. John Kanyetto akieleza kero zinazowakabili wastaafu
Picha ya Pamoja wastaafu wa mkoa wa Dodoma,Mkurugenzi mkuu SSRA, na mkuu wa Hazina ndogo mkoani dodoma Bw. Evance Assenga.
Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii (SSRA) imekutana na Wastaafu wa mkoa wa Dodoma.Wastaafu hao walikutana na uongozi wa Mamlaka ili kuelezea mafanikio na kero wanazokabiliana nazo katika malipo yao ya Pensheni.
Wastaafu hao walimueleza mkurugenzi mkuu wa SSRA Bi.Irene Isaka kuwa Pensheni wanazolipwa ni ndogo sana ikilinganisha na hali halisi ya uchumi nchini.Wastaafu hao waliomba pensheni zipandishwe kulingana na thamani ya shilingi na pia sambamba na upandaji wa kima cha chini cha mshahara.
Wastaafu waliipongeza Hazina kwa kutatua baadhi ya kero zao, kwani kero nyingi walizosiwasilisha katika kikao chao cha mwisho zimetatuliwa.
Pia waliipongeza Serikali kupitia Wizara ya kazi na Ajira na waheshimiwa wabunge kwa kupitisha muswada wa mabadiliko ya sheria za mifuko ya hifadhi ya Jamii, kwani kwa kupitisha muswada huo wana imani kubwa kuwa Mamlaka imepewa meno nayo itafanya kazi kikamilifu na kuboresha pensheni,huduma na mafao yatolewayo na mifuko ya Hifadhi ya jamii.
Picha kwa Hisani ya Michuzi Blog
Picha kwa Hisani ya Michuzi Blog
0 comments:
Post a Comment