Home » » KUTOKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO.

KUTOKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO.


Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira Dkt. Makongoro Mahanga(kushoto) akibadilishana
mawazo na Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige  wakati wa mapumziko
ya mchana ya Bunge la Bajeti  linaloendelea mjini Dodoma.
 
Baadhi
ya wabunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakijaza fomu za
vitambulisho vya Taifa leo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Waziri
Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda(katikati) akibadilishana mawazo jana  na
Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (kushoto) MBUNGE wa Same
Mashariki, Anne Kilango Malecela (kulia),wakati wa mapumziko ya mchana
ya kikao cha Bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
Wakufunzi
wa Sensa ya Watu na Makazi ngazi ya kitaifa wakishiriki katika mafunzo
ya  kujaza dodoso fupi la sense ya watu na makazi leo katika mafunzo ya
siku 10 yanayoendelea mjini Dodoma. Mafunzo hayo yameandaliwa na ofisi
ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakufunzi hao ili nao
waweze kuendesha katika ngazi za mikoa mbalimbali hapa nchini.

Mbunge
wa Mbeya Mjini joseph Mbilinyi (SUGU) akibadilishana mawazo na Mbunge
Mwenzie kutoka Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe leo wakati wa
mapumziko ya mchana ya Bunge la Bajeti  linaloendelea mjini Dodoma.

(Picha na
Tiganya Vincent- MAELEZO-Dodoma).

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa