Home » » CHAMA CHA SOKA WILAYA DOM, YAZITAKA TIMU ZINAZOSHIRIKI LIGI KUZINGATIA NIDHAMU

CHAMA CHA SOKA WILAYA DOM, YAZITAKA TIMU ZINAZOSHIRIKI LIGI KUZINGATIA NIDHAMU

Masoud Masasi,Dodoma
LIGI taifa ngazi ya Wilaya ya Dodoma mjini inatarajiwa kuanza kutimua wiki ijayo katika viwanja viwili tofauti mjini hapa ambapo jumla ya timu 20 zitashiriki mashindano hayo huku chama cha soka wilaya hiyo ikihimiza nidhamu pamoja kuzitaka timu kuwa na walimu wenye taaluma ya ukocha.
Timu za Area A na Gwasa Fc zinatarajiwa kufungua pazia la mashindano hayo katika mchezo wao utakaochezwa katika uwanja wa Magereza mjini hapa ikiwa ni mchezo wa ngao ya hisani.
 Katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Dodoma mjini(Dufa)Said mohamedi alisema timu hizo zimepangwa katika makundi mawili.
Alisema kuwa vilabu vyote vinatakiwa kufuata maelekezo waliyowapa ikiwemo kila timu iwe na mwalimu mwenye taaluma ya ukocha ambapo amesema timu ambayo aitakuwa na kocha mwenye sifa hizo basi haitashiriki ligi hiyo.
“Kama tulivyokubaliana safari hii kama timu haitakuwa na mwalimu mwenye angalau kozi ya awali ya ukocha basi haitoshiriki kabisa ligi kwa kuwa tunataka kutoa timu imara safari hii kwenye wilaya yetu”alisema Mohamedi.
Katika hatua nyingine katibu huyo alizitaka timu zitakazoshiriki ligi hiyo kuzingatia nidhamu na kutoa angalizo kuwa hawatosita kuzifuta timu zitakazoonyesha utovu wa nidhamu katika ligi hiyo.
“Kwa kweli sasa tutakuwa wakali sana hasa kwa  timu ambazo zitakuwa na nidhamu tutazifuta kabisa kushiriki mashindano yoyote yale hapa wilayani kwetu hivyo timu zote zizingatie nidhamu hasa kwenye benchi la ufundi wao ndio vinara wa kuanzisha fujo”alisema katibu huyo.Masoud Masasi,Dodoma
LIGI taifa ngazi ya Wilaya ya Dodoma mjini inatarajiwa kuanza kutimua wiki ijayo katika viwanja viwili tofauti mjini hapa ambapo jumla ya timu 20 zitashiriki mashindano hayo huku chama cha soka wilaya hiyo ikihimiza nidhamu pamoja kuzitaka timu kuwa na walimu wenye taaluma ya ukocha.
Timu za Area A na Gwasa Fc zinatarajiwa kufungua pazia la mashindano hayo katika mchezo wao utakaochezwa katika uwanja wa Magereza mjini hapa ikiwa ni mchezo wa ngao ya hisani.
 Katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Dodoma mjini(Dufa)Said mohamedi alisema timu hizo zimepangwa katika makundi mawili.
Alisema kuwa vilabu vyote vinatakiwa kufuata maelekezo waliyowapa ikiwemo kila timu iwe na mwalimu mwenye taaluma ya ukocha ambapo amesema timu ambayo aitakuwa na kocha mwenye sifa hizo basi haitashiriki ligi hiyo.
“Kama tulivyokubaliana safari hii kama timu haitakuwa na mwalimu mwenye angalau kozi ya awali ya ukocha basi haitoshiriki kabisa ligi kwa kuwa tunataka kutoa timu imara safari hii kwenye wilaya yetu”alisema Mohamedi.
Katika hatua nyingine katibu huyo alizitaka timu zitakazoshiriki ligi hiyo kuzingatia nidhamu na kutoa angalizo kuwa hawatosita kuzifuta timu zitakazoonyesha utovu wa nidhamu katika ligi hiyo.
“Kwa kweli sasa tutakuwa wakali sana hasa kwa  timu ambazo zitakuwa na nidhamu tutazifuta kabisa kushiriki mashindano yoyote yale hapa wilayani kwetu hivyo timu zote zizingatie nidhamu hasa kwenye benchi la ufundi wao ndio vinara wa kuanzisha fujo”alisema katibu huyo.

0 comments:

Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa