Home » » UFUNGUZI WA WIKI YA WAHANDISI MKOA WA DODOMA‏

UFUNGUZI WA WIKI YA WAHANDISI MKOA WA DODOMA‏

 Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) mkoa wa  Dodoma  Maria Sasabo (kulia) akimwunyesha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kushoto) Televisheni ya Digitali na ile ya Analojia ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu juu ya mabadiliko ya Mfumo wa utangazaji toka Analojia kwenda Digitali wakati wa sherehe za ufunguzi wa wiki ya wahandisi Kimkoa katika Viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma jana.Picha na Masoud Masasi
 Mtaalamu wa Miundombinu na Mifumo ya Usambazaji maji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mjini Dodoma (DUWASA)  Revocatus Nsubile akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba) vifaa vinavyotumika katika usambazaji maji wakati wa sherehe za ufunguzi wa wiki ya wahandisi Kimkoa katika Viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma jana Picha na Masoud Masasi.

 Mhandisi Mazingira wa Manispaa ya Dodoma  Barnabas Faida (Kushoto) akitoa maelezo ya kitaalamu kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) juu ya utafutaji wa maji kwa vyanzo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa wiki ya wahandisi katika viwanja vya Nyerere Dodoma jana Picha na Masoud Masasi

Mhandisi Ujenzi wa Manispaa ya Dodoma Lusako Kilembe (kushoto) akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi michoro ya ramani ya mradi wa Ujenzi wa barabara za lami zinazojengwa katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa wiki ya wahandisi katika viwanja vya Nyerere Dodoma jana Picha na Masoud Masasi.







0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa