Home » » CCM DODOMA YAPATA VIONGOZI WAPYA AKIWEMO MWENYEKITI MPYA ADAM KIMBISA‏

CCM DODOMA YAPATA VIONGOZI WAPYA AKIWEMO MWENYEKITI MPYA ADAM KIMBISA‏


Mkoa wa Dodoma umepata mwenyekiti mpya ndugu Adam Kimbisa atakaye kiongoza Chama kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Ndugu Kimbisa amepata nafasi hiyo baada ya kupata kura 941 Kati ya kura 1196 zilizopigwa huku mbili zikiharibika.

Katika nafasi hiyo aligombea na wenzake watatu ambao ni mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Dodoma ndugu William Kusila aliyepata kura 216 na mwenyekiti mstaafu wa wilaya ya Dodoma mjini ndugu Denis Bendera aliyepata kura 30.
Akizungumza mara baada ya matokeo kutangazwa ndugu Kimbisa amewataka wanachama kuvunja makundi yaliyokuwepo wakati wa kampeni ili kwa pamoja waweze kujenga chama.

Awali akifungua mkutano huo wa uchaguzi Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi ambaye ndie aliyekuwa msimamizi mkuu aliwataka wananchi kuelewa kuwa CCM sio ngazi ya kupanda ili mtu apate uongozi kama ambavyo wengine wanadhani.
Amewataka wanaodhani hivyo kuelewa kuwa CCM sio chama cha kukimbilia Pindi watu wakitaka uongozi.
Leo kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kinaketi kwa ajili ya kuchagua Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Mkoa na Katibu wa Fedha na Uchumi.

Ambapo mpaka sasa matokeo yamekuwa ni katibu itikadi na uenezi wa mkoa amechaguliwa Donald Mejiti na katibu wa uchumi na fedha amechaguliwa Mohamedi Rashid Morama.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa