Home » » MWENYEKITI WA CCM TAIFA RAIS KIKWETE AWAONYA UVCCM

MWENYEKITI WA CCM TAIFA RAIS KIKWETE AWAONYA UVCCM


Meza kuu ikiwa na bango lenye ujumbe mzito kutoka katika nukuu za Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Katibu wa Halmashauri kuu Taifa (NEC) Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Mhe. January Makamba akisalimiana na wageni waalikwa kutoka katika jumuiya za vijana vyama mbalimbali kusini na afrika ya kati.

Makatibu wa halmashauri kuu (NEC) kutoka Kulia Uchumi na Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Mhe. January Makamba na Itikadi na Uenezi Ndugu. Nape Nnauye.

Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ambao pia ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM.

Vijana mbalimbali ambao wanawakilisha mikoa wakiwa na mabango ambayo yanaonyesha Mikoa wanayotoka.

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama hicho ambao walimpokea akiwa anaingia katika ukumbi wa mkutano wa nane wa vijana wa chama cha mapinduzi.

Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ndugu Benno Malisa  akimueleza jambo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Jakaya Kikwete katika Mkutano huo.


Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wanaendelea na Mkutano Mkuu wa Taifa ambapo wanatarajia kuchagua viongozi mbalimbali katika ngazi ya Taifa ya jumuiya hiyo, ambapo jumla ya wagombea 133 wamejitokeza kuwania nafasi hizo ambazo ni nafasi ya Mwnyekiti, Makamo Mwenyekiti, Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) kupitia jumuiya ya vijana, ambapo nafasi (6) zinatoka bara na (4) zinatoka Tanzania Visiwani, nafasi nyingine ni Baraza Kuu Taifa, Viti 5 Bara na 5 Zanzibarm Nafasi ya Uwakilishi WAZAZI Taifa na mwisho ni nafasi ya uwakilishi UWT Taifa.


Mkutano Mkuu huo wa UVCCM umefunguliwa Na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, ulianza Rasmi, saa 4 asubuhi, ambapo Mhe. Rais alifanya ufunguzi kwa Hotuba makini, iliyoeleza mambo makubwa na ya msingi juu ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).


Mhe. Jakaya Kikwete alisisitiza na kukumbusha juu ya Lengo kuu na Dhumuni Kuu la Chama Cha Mapinduzi lililotajwa katika katiba yake Ibara ya 5 ambayo inaeleza bayana kuwa ni kushinda uchaguzi na kushika dola.


Lakini pia akaeleza kuwa CCM kinategemea jumuiya yake hiyo kufanya kazi ya siasa miongoni mwa vijana wa Tanzania na kushawishi wakubali kuwa wanachama na wapenzi wa CCM. Akasisitiza kuwa matumaini makubwa ya msingi kuliko yote ya Chama Cha Mapinduzi ni kuona jumuiya yake hiyo inakuwa MKOMBOZI wa vijana.


 Mhe. Kikwete akawataka wahakikishe kuwa wanapata Viongozi ambaowataongoza vyema, watakaoongoza juhudi za kuendeleza, kutetea na kulinda maslahi ya CCM. Viongozi wanaoijua na kuipenda jumuiya ya Vijana.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa