HALI ya uhaba wa
mvua katika Mkoa wa Dodoma, hasa Wilaya ya Chamwino, imemlazimu Mkuu wa Wilaya
hiyo, Fatma Ally, kuja na mbinu mbadala ya kuwataka wananchi wake kugeukia
ufugaji wa kuku kama njia ya kuepukana na baa la njaa, linaloweza kuinyemelea
wilaya hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari wilayani hapa baada ya kutoa mafunzo ya ufugaji kuku kwa wananchi, alisema kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, mvua nyingi za msimu zilizokuwa zinanyesha kwa wakati zimekata, hali inayoweza kutishia kutokea kwa baa la njaa.
DC Fatma, alisema kuwa katika kuhakikisha mkakati huo na utekelezaji wake, amelazimika kuanzisha mradi wa ufugaji wa kisasa wa kuku wa nyama na mayai, bata pamoja na mbuzi, kama mfano kwa wananchi wa wilaya yake.
Alisema mafunzo hayo ameyatoa kwa kuwashirikisha wananchi wa vijiji vya Ikowa, Msamalo, Chamwino na Buigiri, ambayo maeneo yao ni kame, hali iliyosababishwa na kukosekana kwa mvua.
Alisema hali ya ukosefu wa mvua kwa wakati imechangia ukame na mazao kukauka na wananchi kukosa chakula cha uhakika, jambo ambalo si zuri.
“Katika kuhakikisha wananchi wangu hawakumbwi na baa hili la njaa, ni lazima wafuge kuku, kwani ni mtaji mdogo tu unaohitajika ili kuweza kufuga kuku hao, ambao wataweza kujipatia kipato, ikiwa ni pamoja na kuondokana na njaa na kuacha kuomba chakula cha msaada kama ilivyozoeleka,” alisema DC Fatma.
Alisema kuwa soko la kuku ni kubwa endapo wananchi hao watafuga kisasa na kuwatumia wataalamu wa ufugaji wa kuku, ambao hutoa mafunzo bora.
Kwa upande wake, mmoja wa wafugaji hao waliopatiwa mafunzo hayo ya ufugaji kutoka Kata ya Ikoa, wilayani hapa, ambaye pia ni Katibu wa wakulima, Lucy John, aliwaasa wanakijiji wenzake kuacha utegemezi kwa kutafuta mbinu mbadala kupitia sekta ya ufugaji kuku.
Katibu huyo alisema kuwa wananchi hao wamekuwa tegemezi na hawapendi kujishughulisha katika ufugaji, wamekuwa wakipenda kuletewa tu na si kujitafutia wenyewe.

Chanzo: Rai
0 comments:
Post a Comment