Serikali
imepiga marufuku wananchi kufanya shughuli zote za kibinadamu
pembezoni mwa hifadhi zaareli ikiwemo kujenga nyumba, kulima au kufanya
biashara na kuagiza watu wote ambao wanajihusisha na shughuli hizo
kuondoka haraka iwezekanavyo katika maeneo hayo ili kuepusha uharibifu
wa reli na madaraja unaochangiwa watu hao na kulisababishia taifa hasara
kumbwa.
Kauli
hiyo ya saerikali inatolewa na naibu waziri wa uchukuzi Mhe Charles
Tizeba wakati akifanya ziara ya kutembelea madaraja ya treni yaliyopo
wilayani Bahi mkoani Dodoma ambapo amesema shuguliza kubinadamu
zinazofanyika pembezoni mwa hifadhi za reli zikiwemo kilimo na kupitisha
mifungo juu ya reli zinaweza kusababisha reli na madaraja kusombwa na
maji kipindi cha mvua.
0 comments:
Post a Comment