Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa tatu kutoka
kulia), akiongea na fundi ambaye anafanya shughuli za ujenzi katika
Daraja la Reli la Bahi-Kintinku. Dk. Charles Tizeba amefanya ziara
kwenye daraja hilo na kupata taaarifa kuwa limekamilika kwa asilimia
98. Aidha daraja hilo limegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 3.5.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa pili kutoka
mbele), akishuka chini ya daraja la bahi-kintinku kuangalia maendeleo ya
ujenzi wake. Daraja hilo linajengwa na Kampuni ya China Civil
Engineering Construction Corporation(CCECC). Kukamilika kwa daraja hilo
kutasababisha Treni za abiria na mizigo kupita kwa uhakika majira yote
ya mwaka.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, akitoa maelekezo kwa
Mhandisi Mkazi wa mradi kutoka kampuni ya China Civil Engineering
Construction Corporation(CCECC), Bw. Wang Chao(aliyevaa fulana ya rangi
ya karoti), wakati alipotembelea mradi huo mapema wiki hii. Ujenzi wa
daraja hilo umekamilika kwa asilimia 98 na litakabidhiwa kwa Serikali
mapema tarehe 28 Novemba 2013.
Mafundi
wakiendelea na ukamlilishaji wa daraja la Reli la Bahi-kintinku kama
walivyokutwa mapema wiki hii katika eneo la bahi mkoani Dodoma. Daraja
hilo ambalo lina tani 32 litawezesha treni la Abiria na mizigo kupita
kwa majira yote kwa uhakika.
Muonekano
wa daraja la reli linalojengwa na kampuni ya China Civil Engineering
Construction Corporation(CCECC) katika eneo la Bahi mkoani Dodoma.
Kukamilika kwa daraja hilo kutawezesha treni ya reli ya kati kupita kwa
majira yote ya Mwaka. Aidha daraja hilo limekamilika kwa asilimia
98.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
0 comments:
Post a Comment