Dodoma. Wajasiriamali nchini wametakiwa kutumia
mafunzo wanayoyapata kwa njia mbalimbali kuboresha bidhaa zao ili
waweze kushindanisha bidhaa zao katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Chamwino, Adrian Jungu, alipokuwa akifunga maonyesho ya wajasiriamali
wa bidhaa za ngozi yaliyoandaliwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda
Vidogo Vidogo (Sido), mkoani hapa.
“Mtumie mafunzo yenu katika kuondoa upungufu wenu
katika bidhaa mnazozitengeneza ili kuziboresha na hivyo kuongeza
ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi,” alisema Jungu.
Akimkaribisha kufunga maonyesho hayo, Meneja wa
Sido mkoani hapa, Abeil Mapunda, alisema wajasiriamali wanane wamepata
mafunzo katika kituo hicho cha mafunzo ya kutengeneza bidhaa za ngozi
cha Kizota mjini hapa.
Alisema wajasiriamali hao walipata mafunzo ya wiki
tatu ya kutengeneza mikanda, pochi za simu na viatu. “Kituo kilianza
kutoa mafunzo mwaka 2011 na watu zaidi ya 200 wamenufaika na mafunzo,”
alisema Mapunda.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment