Home » » Makampuni ya ulinzi yatakiwa kusajiliwa na TSIA

Makampuni ya ulinzi yatakiwa kusajiliwa na TSIA

Makampuni ya ulinziSERIKALI imeombwa kuyaagiza makampuni ya ulinzi kujisajili katika Chama cha Sekta ya Ulinzi Nchini (TSIA) kabla hayajaanza kazi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa TSIA Almas Maige wakati akisoma risala ya chama hicho katika mkutano mkuu wa mwaka.
Maige alieleza kuwa awali utaratibu wa kusajili makampuni ulikuwa ukihakikiwa kwa pamoja kati ya Jeshi la Polisi  na TSIA.
Alisema hali hiyo hivi sasa imetoweka kwani Jeshi la Polisi limekuwa likisajili makampuni ya ulinzi bila kushirikisha TSIA, hivyo kutoa mwanya kusajiliwa kwa makampuni uchwara na ya ubabaishaji na hata mengine kumilikiwa na wahalifu.
“Sisi tunawafahamu wadau wote wa sekta lakini pia tunatunza taarifa za aina zote za taaluma za sekta ya ulinzi,’’ alisema mwenyekiti huyo.
Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dodoma Damas Nyanda alisema ni muhimu kwa makampuni hayo kufuata utaratibu katika utendaji wa kazi zake.
Aidha alisema kwamba Jeshi la Polisi linatambua umuhimu na kazi kubwa inayofanywa na makampuni hayo kwani yamekuwa msaada mkubwa kwa jeshi hilo katika kutoa ulinzi kwa raia na mali zao.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa