Home » » Wafugaji wavamia ofisi za CCM

Wafugaji wavamia ofisi za CCM

KUNDI la wawakilishi wa wafugaji kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, limetinga katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makao Makuu mjini hapa ili kupeleka kilio chao cha kunyanyaswa na askari wanaofanya kazi ya operesheni tokomeza.
Wafugaji hao waliokuwa wameambana na Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda (Chadema), juzi walipeka kero zao kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu operesheni hiyo inayopambana na majangili na ile ya kuondoa wahamiaji haramu.

Wakiwasilisha malalamiko yao mbele ya Kinana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi pamoja na Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Benedict Ole Nagoro, ambapo walisema kuwa hivi sasa wamekuwa kama wakimbizi kutokana na operesheni hizo.

Akijibu malalamiko hayo ya wafugaji Kinana, alisema kuwa wamelipokea suala hili huku akiahidi kulishughulikia kwa kuitaka Serikali kukaa na kutafakari kwa kina namna ya kuondoa changamoto hizo zinazojitokeza.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Benedict Ole Nangoro, alisema kuwa wafugaji ni watumiaji wa ardhi tu lakini Wizara hiyo haina jukumu la kutatua suala hilo na hivyo kurusha mpira kwa Wizara nyingine kwa madai kuwa wanatakiwa wakae wote washirikiane waone namna ya kutatua tatizo hilo.

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema kuwa Serikali kupitia wizara zote zinazohusika katika kazi hiyo zitakutaka na kuweza kujadili kwa kina changamoto hizo ili kuweza kuzipatia ufumbuzi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa