Home » » WAFUGAJI WILAYANI BAHI WAONYWA KUPITISHA MIFUGO YAO KATIKATI YA BARABARA

WAFUGAJI WILAYANI BAHI WAONYWA KUPITISHA MIFUGO YAO KATIKATI YA BARABARA


 Kiongozi wa kikundi kimojawapo cha vikoba katika kijiji cha Nagulo Elfrida Matonya akipokea msaada wa jembe la kukokotakwa mkono toka mfuko wa jimbo uliotolewa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi Philemon Mdate kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Bahi Omary Baduwel.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bahi Philemon Mdate akimkabidhi muwakilishi wa kikundi cha vikoba kilichopo katika kijiji cha Nagulo Sevelin Mtemba Jembe la kukokota kwa mkono lenye thamani ya 200,000 lililotolewa na mbunge wa jimbo la bahi Omari Baduwel toka kwenye mfuko wa jimbo.
 Mwenyekiti wa CCM wilayani Bahi mkoani Dodoma Philemon Mdete Akiwa na baadhi ya viongozi walipokuwa wakagua Barabara ya Bahi Nagulo iliyokamili yenye ulefu wa Km. 6
 Barabara hiyo iliyomalizika kuchongwa kwa kiwango cha Changalawe inavyoonekana baada ya kukamilika.
 Pamoja na mwenyekiti huyo kupiga marufuku mifugo kutokatiza barabara hiyo bila utaratibu mbuzi wanapita wakati hata hajamaliza kuikagua barabara hiyi iliyo kaktika kiwango cha changalawe.
Wanachi wa kijiji cha Nagulo wakiwa kwenye mkutoo wa hadhara uliohutubiwa na mwenyekiti wa CCM walaya ya Bahi mara baada ya mwenyekiti huyo kumaliza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kijijini hapo.
Na John Banda, Bahi

WAKAZI wa kijiji cha nagulo wameonywa kutopitisha mifugo yao katika barabara bila mpangilio maarumu uliowekwa na uongozi wa kijiji hicho la sivyo watatozwa faini kali.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bahi Mkoani Dodoma Philemon Mdate alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.

Mwenyekiti huyo alisema kumekuwa na upitishaji holela wa mifugo katika maeneo mengi ya barabara wilayani humo hali ambayo imekuwa ikichangia uhalibifu mkubwa ikiwemo mashimo huku usalama wa mifugo yenyewe ukiwa hatarini.

Mdate alikuwa akisisitiza hilo mara baada ya kumaliza kuitembelea barabara  iliyomalizika
kujengwa katika kijiji hicho cha nagulo kwa yenye ulefu wa KM. 6 kwa kiwango cha changalawe, huku akiwataka afisa mtendaji na Mwenyekiti wa kijiji hicho kuhakikisha wanatenga na ijengea kuwa njia pekee ya kupitishia mifugo.

‘’Ili kuepusha uhalibifu wa barabara mwenyekiti na mtendaji tengeni eneo na mlijenge ili mifugo yote ipitishwe hapo na mtu yoyote atakaekiuka atatozwa faini isiyopungua 5000 kwa ng’ombe mmoja na mbuzi mmoja 2500 na msiwe na huruma kwa mtu’’, alisema

Aidha aliwataka wananchi wote wa kijiji hicho kuilinda barabara hiyo kutokana na kujengwa kwa gharama kubwa ya 71.6 milioni, hivyo watoe ushirikiano wa kutoa taarifa kwa viongozi wao.

Katika ziara hiyo  Mwenyekiti huyo wa CCM Bahi alitembelea miradi mingine ya Afya, Elimu na ofisi ya serekali ya kijiji iliyojengwa kutokana na nguvu na gharama za wakazi wa kijiji hicho.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa