Dodoma. Serikali imekiri kuwapo wanaume ambao
mbegu zao hazina uwezo wa kuwapa mimba wanawake na kwamba, imekuwa
ikiendelea kutoa elimu mara kwa mara.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alipojibu swali la nyongeza la Mbunge wa
Viti Maalumu, Kidawa Saleh (CCM).
Mbunge huyo alitaka kujua iwapo Serikali haioni
umuhimu wa kutoa elimu kwa wanaume ili wajue wapo ambao mbegu zao hazina
uwezo wa kumpa mwanamke mimba na kwamba, tatizo hilo siyo kwa wanawake
pekee.
“Kwa kuwa wanawake wengi wamekuwa wakiiba watoto
kutokana na kunyanyaswa na waume zao kwa kutokuwapatia watoto, je
Serikali kwa nini isitoe elimu kwa wanaume?” alihoji mbunge huyo.
Dk Seif alikanusha kuwa siyo wanawake pekee wenye
matatizo ya kushindwa kushika mimba, bali zipo sababu kwa pande zote
mbili za kushindwa kutunga mimba.
Alisema wamekuwa wakitoa elimu ya uzazi mara kwa mara vituo vya tiba na kupitia vyombo vya habari, kuhusu jambo hilo.
Awali, katika swali la msingi, Kidawa alitaka kujua sababu za kuongezeka kwa tatizo hilo miaka ya karibuni.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuanzia Januari, 2011 hadi Septemba
mwaka huu kulikuwa na matukio 310 ya wizi wa watoto nchi nzima, kati yao
wa kike ni 128 na wa kiume 182.
Alisema watoto 177 kati ya 310 walioibwa, walipatikana baadhi yao wakiwa hai.
na wengine wakiwa watuhumiwa 174 wakiwemo wanaume 101 na wanawake 73 walikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment