Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWENYEKITI wa Bunge Maalumu la Katiba, Bw.
Samuel
Sitta amewataka wajumbe wa Bunge hilo kuchagua Mwenyekiti mwenye uwezo
wa kuongoza kamati zao aweze kuwasilisha maoni yao.
Bw. Sitta
aliyasema hayo bungeni Mjini Dodoma jana kwenye kikao cha Bunge hilo
wakati wa mchakato wa kupanga kamati ambazo zitajadili vifungu vya
Rasimu ya Katiba.
Alisema katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu wake kwenye kamati husika ni vyema wajumbe wakazingatia sifa
ya mjumbe ambaye watamchagua bila kujali ushabiki wa vyama ili aweze kuwasilisha maoni yao kuhusu rasimu hiyo.
Kamati
12 ziliundwa ambapo hadi jana jioni, kila kamati ilipaswa kufanya
uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu wake pamoja na kupangiwa eneo la kudumu
kwa ajili ya kukutana.
Alisema kazi ya kamati hizo ni kujadili ibara
za rasimu na kuziwasilisha bungeni ambapo kila moja ina wajumbe 52
wakati Kamati ya Uandishi wa Kanuni na ile ya Kanuni na Haki za Bunge
kila moja ina wajumbe 24 ambao wameteuliwa kutoka kwenye kamati 12 ambazo zimeundwa.
Bw. Sitta aliongeza kuwa, uteuzi wa wajumbe wa kamati hizo umezingatia vigezo vilivyowekwa kwenye kanuni ikiwemo jinsia,
pande za Muungano, wajumbe 201 wa kuteuliwa, kutoka Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamhuri ya Muungano.
“Tunataka
kuweka utaratibu ili katika sura zisizo na matatizo, tutashughulikia
sura tatu au nne kwa pamoja ili tuweze kumaliza katika muda ulioelezwa
kwa mujibu wa sheria, hatuwezi tukakaa hapa mwaka mzima,” alisema Bw.
Sitta.
Alisema ataunda Kamati ya Uongozi baada ya kamati 12 kuchagua
viongozi wao ambapo Kamati ya Mashauriano itaundwa kutokana na
majadiliano jinsi yatakavyokuwa yakiendelea.
Wakati huo huo, mwezeshaji kwenye simina ya waandishi wa habari kuhusu wajibu walionao
katika kuripoti habari za Bunge hilo, Dkt. Ayub Rioba, amewataka waandishi kuandika habari za
Bunge la Katiba kwa lugha nyepesi na inayoeleweka kwa wananchi.
Alisema
taarifa za Bunge hilo zina umuhimu na manufaa makubwa kwa wananchi
hivyo zinapaswa kuandikwa kwa umakini bila kutunga uongo ili kutochochea
mitafaruku.
“Hatupaswi kuandika habari zinazoweza kuuvuruga mchakato
huu kwa sababu ya kufanya biashara...epukeni kulazimisha maoni binafsi
ya vyombo vyenu ili yaonekane ndio mwelekeo wa Bunge la Katiba,” alisema
Dkt.
Rioba.
Naye Mwalimu Bashiru Ally, kutoka Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM), aliwataka wajumbe wa Bunge hilo kuhakikisha
wanatekeleza dira ya ukombozi kwani ndiyo iliyowaongoza wapigania uhuru
barani Afrika kudai haki ya kujitawala.
Alisema ni muhimu wajumbe wa
Bunge hilo wakaitumia vizuri Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Kanuni za
Bunge hilo, rasimu na ripoti za Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwani
nyenzo hizo ndio zilizozaa hotuba ya Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji
mstaafu Joseph Warioba na Rais Jakaya Kikwete.
“Hotuba za viongozi hawa ni nyenzo muhimu kwa wajumbe wa Bunge hili ambao wanapaswa
kujenga
msingi wa maridhiano kwa kuhakikisha yaliyomo kwenye nyaraka zote hizo
yanawaongoza vyema kwani nyaraka hizo zimeandaliwa ili kuwapa mwanga,”
alisema Mwalimu Ally.
Viongozi wa kamati Waliochaguliwa kwenye kamati namba moja, Mwenyekiti UmmyMwalimu, Makamu wake Profesa Makame Mbalawa, kamati
namba
mbili Mwenyekiti Shamsi Vuai Nahodha, Makamu wake Shamsha Mwangunga,
namba tatu Mwenyekiti Francis Michael, Makamu wake ni Fatuma Mussa Juma.
Kamati namba nne Mwenyekiti Christopher Ole Sendeka, Makamu wake Dkt. Sila Ugwa, namba
tano
Mwenyekiti Hamad Rashid, Makamu wake, Assumter Mshama, namba sita
Mwenyekiti Stephen Wassira, Makamu wake ni Dkt. Maua Daftrari.
Namba saba Mwenyekiti Hassan Ngwilizi, Makamu wake Waride Bakari Jabu, namba nane
Mwenyekiti Job Ndugai, Makamu wake Biugwa Yahya Othuman, namba tisa Mwenyekiti Kidawa
Hamisi Salehe, Makamu wake Wiliam Ngereja.
Kmati namba 10, Mwenyekiti ni Anna Abdallah, Makamu wake Salmin Awadh Salmin, namba
11, Mwenyekiti Anne Kilango Malecela, Makamu wake Yusuph Masaluni, namba 12 Mwenyekiti
Paul Kimiti, Makamu wake ni Thauwayba Edinton Kisasi.
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment