Home » » MATUKIO MBALI MBALI KUTOKA BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO

MATUKIO MBALI MBALI KUTOKA BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mjumbe wa Bunge Maalum, Evod Mmanda akifafanua kanuni za bunge hilo leo mjini Dodoma.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akizungumza na Mjumbe wa Bunge wa Maalum ambaye pia ni Spika wa Baraza la wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho wakati wa semina ya kuhusu kanuni za bunge hilo leo mjini Dodoma.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi  akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda(kushoto) wakati wa semina ya kuhusu kanuni za bunge hilo leo mjini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria ,Dk. Rose Asha Migiro akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia ,Januari Makamba wakati wa semina ya kuhusu kanuni za bunge hilo leo mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum Dk.  Tulie Akson  akifafanua kanuni za bunge hilo leo mjini Dodoma.
(Picha na Magreth Kinabo)

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa