Home » » IBADA YA KUUOMBEA MWILI WA ALIYEKUWA ASKOFU WA KANISA LA ANGLICAN DAYOYSISI YA KATI GODFREY MHOGOLO YAFANYIKA LEO‏

IBADA YA KUUOMBEA MWILI WA ALIYEKUWA ASKOFU WA KANISA LA ANGLICAN DAYOYSISI YA KATI GODFREY MHOGOLO YAFANYIKA LEO‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Jeneza likiwa na  mwili wa aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Dayosisi ya Dodoma Godfrey Mdimi Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika ya Kusini alikopelekwa kwa matibabu likiwa ndani ya kanisa kuu la Roho Mtakatifu wakati wa ibada maarumu.
Waumini na viongozi wa kanisa la Anglican Dayosisi ya kati wakilishusha Jeneza lilibeba mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo ulipofikishwa kwa mara ya kwanza tokea alipofariki nchini Afrika ya Kusini kanisani hapo kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya maombezi.
Wachungaji na makasisi wa Kaanisa la Anglican Dayosisi ya Kati wakiwa wamejipanga nje ya kanisa la Roho mtakatifu mjini Dodoma kwa ajili ya kuupokea mwili aliyekuwa Askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo.
  Waumini wa kanisa la Anglican wakiwa kwenye mahema yaliyowekwa nje ya kanisa kuu la Roho Mtakatifu walipokuwa wakifuatilia ibada ya kuuombea mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo kanda ya Dodoma  aliyefariki wiki iliyopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Afrika ya Kusini.
 Wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi wakiwa ndani ya kanisa la Roho Mtakatifu kwa ajili ya ibada maaumu ya kuuombea mwili liyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita alipokuwa kwenye matibabu Afrika ya Kusini.
 Ndani ya kanisa la Roho mtakatifu waumini wakifuatila ibada ya kuuombea mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita akiwa kwenye matibabu.
Baadhi ya Viongozi wa Serekali wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Waumini wa kanisa hilo wakiwa ndani ya hema lilijengwa katika eneo la makaburi ya kuzikia viongozi wa kanisa la Anglican Dayosisi ya kati ambapo walikuwa wakiandaa sehemu ya kuuzikia mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo Godfrey Mhogolo unaotarjiwa kuzikwa kesho Jumamosi.

PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJA BLOG

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa