Home » » Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta akutana na Viongozi wa Dini

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta akutana na Viongozi wa Dini

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

PIX 1
Mhe. Mufti Sheikh Issa Shaaban Simba  akimkaribisha Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta leo jijini Dar es Salaam wakati alipomtembelea kumuelezea maendeleo ya vikao vya Bunge linaloendelea mjini Dodoma.
PIX 3
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta (kulia) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake katika Ofisi za Bakwata kuelezea maendeleo ya cikao vya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Bakwata Suleiman Lolila.(PICHA ZOTE NA BUNGE MAALUM LA KATIBA).
Na. Benedict Liwenga-Maelezo
MWENYEKITI wa Bunge maalum la Katiba Samweli Sitta amesema  katiba mpya ni kwa manufaa ya wanachi wote kwa ajili ya kuwaletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam alipokutana na Mhe. Mufti Sheikh Issa Shaaban Simba   katika Ofisi za Bakwata zilizoko Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kwa ajili ya kuwashirikisha Viongozi wa madhehebu na dini ili nao wapate taarifa ya maendeleo ya bunge la katiba. 
Mhe. Sita amesema kuwa Viongozi wa dini ni watu muhimu sana kwakuwa wanabeba wafuasi wengi katika jamii na kuwepo kwao kunasaidia katika maendeleo ya nchi hususani kujenge Amani ya nchi yetu na kuwahamasisha wananchi kuwa wavumilivu,watulivu,waelewa na wenye kupenda Amani.
Namuomba Mhe. Mufti pamoja viongozi wengine wa dini waizidi kutuombea ili tuweze kufikia muafaka katika kupata katiba mpya na bora yenye kuleta mabadiliko katika nch yetu” Alisema Mhe. Sitta.
Mhe. Sita Ameongeza kuwa Watanzania wanataka katiba itakayoijenga Taasisi imara zitakazoweza kusimamia mambo muhimu na kuweza kuondokana na  uhalifu ikiwemo janga la madawa ya kulevya ambalo limekuwa likiisumbua sana nchii kwa msaada wa sheria mpya janga hili linawezekana kudhibitiwa.
Pia amewaomba wajumbe wa kamati kumi na mbili za bunge la katiba,wasome kwa makiini ibala ya sura ya 1 na ya 6 ambazo ni muhimu sana katika kuijenga nchi, ili waweze kutoka na mawazo mazuri na yakinifu  kwa manufaa ya nchi na watu wake na kuweza kukuza uchumi na kuleta maendeleo.
“Katiba itunge sheria ambazo ni imara zenye kufuata kanuni na taratibu dhabiti ili kuleta mabadiliko katika kuiongoza nchi na kuweza kuwasaidia wananchi wake” Alisema Mhe. Sitta.
Aidha, ameongeza kuwa Bunge hilo maalum linatarajia kuhailishwa mwezi wa nne tarehe 28 kwa ajili ya kupisha bunge la Bajeti,na kwa kuwa siku  70 hazitoshi kumaliza bunge hilo amemuomba Mheshimiwa Rais Kuwaongezea muda hivyo wanatarajia kurudi tena mwezi wa nane kuweza kuendelea na mijadala ya katiba mpya.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa