Home » » MUIMBAJI WA INJILI BAHATI BUKUKU APATA AJALI DODOMA AKIELEKEA KAHAMA KWENYE TAMASHA

MUIMBAJI WA INJILI BAHATI BUKUKU APATA AJALI DODOMA AKIELEKEA KAHAMA KWENYE TAMASHA



Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bahati Bukuku akiwa kwenye moja ya kazi zake ya uimbaji.

Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Gari lenye namba IT 7945 aina ya Toyota Nadia ikiendeshwa na EDSON S/O MWAKABUNGU, Mnyakyusa, Miaka 31 mkazi wa Tabata – Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na kusababisha majeruhi kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari lingine linalosadikiwa kuwa ni Fuso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 majira ya saa 03:00 alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa.

Kamanda MISIME amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni EDSON s/o MWAKABUNGU ambaye analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote, BAHATI D/O BUKUKU, Miaka 40, Mnyakyusa, Msanii wa nyimbo za Injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake na FRANK S/O CHRISTOPHER, Muha, Miaka 20, Msanii wa muziki wa Injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam yeye ana michubuko usoni na mkono wa kulia. Wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Aidha Kamanda MISIME ameongeza kwa kusema kuwa watu walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la Injili.

Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.
Na Jiachie Blog
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa